TAKUKURU YATOA TAARIFA MAALUM KUHUSIANA NA MANENO YA OFISA WAKE KUHUSU RUSHWA NA MAHAKAMA KISUTU LIVE!!
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi
kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU
aliyenukuliwa kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na
hali ya Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili huyo
alinukuliwa akisema kuwa “Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO
Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
Wakili
Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si
msimamo wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na
jamii kwa ujumla itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake
binafsi.
TAKUKURU
ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni
muhimili wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.
TAKUKURU inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake.
IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO,
TAKUKURU MAKAO MAKUU
20 April, 2016
TAKUKURU YATOA TAARIFA MAALUM KUHUSIANA NA MANENO YA OFISA WAKE KUHUSU RUSHWA NA MAHAKAMA KISUTU LIVE!!
Reviewed by The Choice
on
7:36:00 PM
Rating:
No comments: