MAAJABU YA AJALI YA DCM NA ROLI DAR
Ajali ilivyotokea
Na Mwandish wetu, Risasi Jumamosi
DAR
ES SALAAM: Wakati ajali mbaya iliyohusisha magari matatu ikiwa bado
ndani ya vichwa vya watu jijini Dar es Salaam, baadhi ya mashuhuda
wanaelezea maajabu yaliyoambatana na tukio hilo lililotokea Jumatano,
likihusisha daladala aina ya Toyota DCM linalofanya safari zake kati ya
Gongo la Mboto na Ubungo.
Ajali
hiyo ilitokea baada ya daladala yenye namba za usajili T 629 CTT ikiwa
na abiria, kugongwa kwa nyuma na lori aina ya Scania lililokuwa limebeba
mchanga, lenye namba za usajili T 447 DBH na kuifanya daladala hiyo
kupoteza mwelekeo na hivyo kuhama kutoka upande wake hadi wa pili ambako
liligongana na Scania lingine lenye namba za usajili T 109 DDX,
lililokuwa katika mwendo mkali na kusababisha vifo vya watu wanne na
majeruhi 25.
“Nilikuwa
ndiyo naingia barabarani ili niende kupanda gari kituoni (Matumbi),
nikasikia kishindo kikubwa upande ule wa pili, nilipoangalia vizuri
ndipo nikaiona daladala inahamia upande huu, wakati huo lori la ng’ombe
nalo lilikuwa linakuja kwa kasi sana. Katika taa kali za gari, nikawaona
paka wawili wakiwa katikati ya barabara,” anasema Korongo Japhet,
aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Kigogo Dampo.
Alisema
wakati akitafakari kitakachotokea, mara alisikia kishindo kikubwa
kilichofuatiwa na kelele nyingi kutoka kwa wasafiri na watu waliokuwa
kituoni wakisubiri usafiri.
“Lilikuwa
ni tukio la kutisha sana kwa kweli. Sijawahi kukutana na hali hii, mimi
huwa mwoga sana, sikusogea eneo la ajali, nikatembea kwa miguu hadi
Buguruni ambako nilipanda gari kwenda kibaruani kwangu,” alisema shuhuda
huyo.
Shuhuda
mwingine, Zuwena Boaz mkazi wa Tabata Relini, alisema alikuwa akitembea
alfajiri hiyo kuwahi mchicha katika Bonde la Msimbazi wakati aliposikia
kishindo kikubwa mara tu baada ya kuingia barabarani.
“Mimi
nililiona lile DCM likipanda ukuta wa barabara kuhamia upande wa pili,
kitu cha ajabu ninachokumbuka kuona ni njiwa wawili weupe wakiruka juu
ya ile daladala, lakini sekunde chache baadaye sikuwaona wale ndege,
ndipo sasa kikatokea kishindo kingine cha lile lori la ng’ombe,
nakumbuka nilikimbia kurudi nilikotoka, nikarudi baadaye nikiwa
natetemeka sana,” alisema Zuwena.
MAAJABU YA AJALI YA DCM NA ROLI DAR
Reviewed by The Choice
on
11:39:00 PM
Rating:

No comments: