Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.
FAHAMU KUHUSU NDUMBA ZA KICHAWI NA JINSI YA KUJIKINGA NAZO.
Mwandishi : Dokta. Mungwa Kabili….0744 000 473
Nimekuwa
nikipokea barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, wakitaka kujua
masuala mbalimbali kuhusu ulozi, uchawi na jinsi ya kujikinga
dhidi ya uchawi na ulozi.
Kwa kuwa muda na nafasi haviniruhusu kumjibu kila mmoja kwa wakati wake, nitayajibu maswali yote hapa bloguni.
SWALI
: NIMESIKIA KUWA WACHAWI HUWA HAWAFI UPESI.JE KUNA UKWELI
WOWOTE KATIKA HILO ? NA KAMA NI UKWELI, JE NI KITU GANI HUWAPA
UWEZO WA KUISHI MAISHA MAREFU ?
DOKTA. MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Ni
kweli kabisa wachawi wengi huwa hawafi upesi na zipo sababu
kuu mbili zinazo wafanya wachawi waishi muda mrefu :
1.Kwanza
: NDUMBA ZA KINGA: Wachawi wa nchi hutumia ndumba za kinga,
ndumba hizo husaidia kuwakinga dhidi ya shari za wanadamu na
majini wabaya na hivyo kuwafanya waishi siko zote walizo pangiwa
na Mwenyezi Mungu. Ikitokea mchawi mwenye kinga hizo, amefariki
dunia, basi anakuwa amefariki kwa mkono wa Mungu mwenyewe na si
mwanadamu. Watu wengi hufa kwa mikono ya wanadamu waovu na shari
za mapepo wabaya. Nitataja ndumba mbili zenye nguvu zinazo
tumiwa na wachawi.
i. Kuna ndumba moja ya kichawi, ambayo kwa lugha za kisukuma na kinyamwezi hujulikana kama LUFAKALE.
Ndumba
hii ya kichawi akichanjiwa mtu humkinga dhidi ya shari za
wanadamu na mapepo wabaya. Humfanya aishi kwa kadri Mungu
alivyop mkadiria. Humkinga na kumuepusha na shari kama ajali
(hususani ajali za kichawi ), kufa kwa kurogwa nakadhalika.
Ndumba
hii ina nguvu sana kiasi kwamba, mtu aliye chanjiwa , inapofika
siku yake ya kufa roho yake huchukua muda mrefu sana kuacha
mwili wake. Inaweza kumchukua mwaka mmoja hadi miaka kumi. Mtu
anakuwa anonyesha dalili zote za kufa, au anakuwa ameisha kufa
kabisa, lakini anakuwa bado anaongea. Nikipata nafasi siku zijazo
nitaelezea kwa kina kuhusu ndumba hii.
ii.
Ndumba ya pili, inatokana na mti unaitwa Msonihya . Huu ndio mti
mkuu wa wachawi. Mtu huu una nguvu sana za kichawi. Mti huu
hutumika kutengeneza hirizi ambayo huvaliwa mkononi kama bangili
au kuwekwa nyumbani. Hakuna pepo, jinni wala kitu chochote kile
kibaya kinaweza kumdhuru mtu aliye pewa hirizi hii.
Simba , nyoka wa kawaida pamoja na samba & nyoka wa kichawi au mnyama yoyote yule hawezi kumdhuru.
2. NDUMBA ZA KUWAWEZESHA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA MBELENI.
Wachawi
wa nchi wanazo ndumba zenye uwezo wa kuwasaidia kujua mambo
yatakayo tokea mbeleni, hivyo basi kama kuna hatari yoyote ile
inaenda kutokea kesho yake kama vile ajali au shari yoyote ile
nakadhalika, wao wanakuwa wameshajua siku moja kabla na hivyo
wanakuwa na nafasi ya kuchukua tahadhari mapema.
JINSI WANAVYO FANYA ILI KUWA NA UWEZO WA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA.
Zipo
njia mbalimbali wanazo tumia, ili kupata uwezo wa kuona mambo
yatakayo tokea mbeleni, lakini kati ya njia hizo njia ifuatayo
ni maarufu sana miongoni mwa wachawi na walozi.
i. Wanachukua ubongo wa fisi
ii. Wanachukua ubongo wa kunguru
iii.
Wanachukua ubongo wa ndege anaitwa Mbesi. Ndege huyu hupatikana
mtoni na chakula chake kikuu ni mizoga ya ndege, wadudu, samaki
na wanyama. Katika ulimwengu wa wachawi, ndege huyu hujulikana
kama mtaalamu wa kugundua mahali ilipo mizogo iliyo kufa.
Kwa
mfano tuchukulie mkoa wote wa Dar Es Salaam ni pori, huyu
ndege yupo mbagala halafu maeneo ya msasani kuna
ndege,samaki,wadudu au mnyama amekufa, basi usiku wa siku hiyo
ndege huyu ataota mahali ulipo mzoga huo, na kesho yake atapaa
moja kwa moja hadi sehemu ulipo mzoga huo na kuufanya kuwa
kitoweo chake.
Vitu
vyote hivyo hapo juu hukaushwa na kusagwa kwa pamoja na
kisha kuchanganywa na ndumba tatu za kichawi ambazo sitazitaja
hapa kwa sababu maalumu.
Baada ya hapo, mchawi husika atachanjiwa ndumba hizo kichwani pamoja na kwenye zote nne za mwili.
Basi, mchawi huyo anakuwa na uwezo wa kuona ndotoni kila kitu kitakacho tokea kesho yake na kuendelea.
SWALI NAMBA MBILI : NASIKIA WATU WANAZUNGUMZA KUHUSU DUDUMIZI. JE DUDUMIZI NI NINI NA ANATUMIKAJE KATIKA UCHAWI
DR. MUNGWA KABILI ANAJIBU ;
Dudumizi
ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege
hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa
wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya
Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani
mkoani Tanga.
Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.
Dudumizi
wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa
cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba,
Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi
wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye
nyushi nyeupe.
MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU
LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano,
ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa
Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi
unakuta ile kamba imejifungua yenyewe . Ukimnchukua Dudumizi
ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga
kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda
kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta
Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo
itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.
AJABU
LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili
hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko
jike, ndio linalo hatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba
iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe,
ikichanganya na ndumba za kichawi pmaoja na vizimba vyake,
hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali
vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika
mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu,
nakadhalika.
2. Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.
SWALI NAMBA TATU: JE NI KWELI KUWA WACHAWI WANA UWEZO WA KUMTIA MTU MIKOSI NA KUFUNGA RIZIKI YAKE?
DOKTA.MUNGWA KABILI ANAJIBU ;
Ni
kweli kabisa,wachawi wana uwezo wa kumtia mtu mikosi . Zipo
njia mbalimbali wanazo tumia wachawi katika kuwatia watu mikosi,
ila kutokana na ufinyu wa nafasi, nitaelezea moja hapa ;
Katika njia hii, wachawi wakitaka kumtia mtu mikosi, hufanya mambo yafuatayo :
i. Wanachukua hela ambayo haitumiki
ii. Mavi ya mbwa mweusi ambayo ameyanya usiku
iii.Mkaa
ulio kwisha tumika, ambao umetumika mahali ambapo watu hawalali
kama vile kilioni au kwenye bara na migawaha inayo kesha lakini
mara nyingi, huchukua mkaa wa kilioni.
iv.
Mavi ya ndege anaitwa Mumbi. Huyu ndege aitwae Mumbi
anapatikana porini. Anafanana sana na bata na ana puyanga la
rangi nyekundu.
v.Shahidi la kaburini pamoja na ndumba zingine za kichawi
vi.Kitu
chochote cha mtu aliye kusudiwa kutiwa mikosi kama vile picha
yake, mchanga alipokanyagia, mate, kucha, au chochote kile.
Baada
ya hapo, mchawi huyo atakwenda kaburini usiku wa manane na
kuvizika vitu vyote nilivyo vieleza hapo juu, huku akisema
maneno ya kichawi ambayo siwezi kuyataja hapa. Basi mtu aliye
kusudiwa na uchawi huu, kama hana kinga, ata andamwa na mikosi
mikubwa na mizito katika maisha yake yote.
SWALI NAMBA NNE : DOKTA, NINAPENDA KUJUA NINI KINGA DHIDI YA UCHAWI? NIFANYE NINI ILI UCHAWI USINIDHURU ?
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU:
Kama
wewe ni Muislamu, uwe mtu wa swala sana, kufanya duwa na visomo (
Ruqiya) na kutoa Dhaka na swadaka kwa mola wako, na kama wewe
ni Mkristo, basi uwe mtu wa kusali sana, kufunga na kuomba bila
kusahau kutoa sadaka na fungu la kumi kwa Mungu wako.
Lakini kama unajijua, hauwezi kufanya mambo niliyo yataja hapo juu, basi unatakiwa kupata kinga ya mwili wako.
Zipo
kinga nyingi zenye nguvu dhidi ya uchawi na ulozi. Zipo Kinga,
mchawi akikutupia uchawi unamrudia mwenyewe ana kufa papo hapo
au anapooza kwanza kwa muda mrefu kisha anakufa pia zipo kinga
ambazo mchawi , akitaka kukutupia uchawi, anashindwa kukuona
katika rada zake za kichawi.
Hii ni kinga muhimu sana na haiishii kukukinga mwili wako pekee.Inakinga nyumba, biashara, kiti cha ofisi nakadhalika.
KINGA HII HUJULIKANA, KAMA KINGA YA KUFICHA KIVULI CHAKO.
Inaitwa
Kinga ya Kuficha kivuli, kwa sababu wachawi wanapo taka kumloga
mtu, huchukua na hushambulia kivuli chake. ( HAPA SIZUNGUMZII
KIVULI CHA JUANI, NAZUNGUMZIA KIVULI CHAKO CHA KIROHO, YAANI
NAFSI YAKO )
Bila kuona kivuli chako, wachawi hawawezi kukuloga.
Kinga
hii hukupa uwezo wa kutokuonekana kwenye rada za wachawi. Kwao
unakuwa ni sawa na mtu aliye kufa tu, kwa sababu mtu aliye
kufa kivuli chake hakionekani na pia hawezi kurogwa na uchawi
wa aina yoyote ile.
JINSI YA KUFICHA KIVULI CHAKO KISIONEKANE NA WACHAWI.
i. Chukua nywele za saluni
ii. Chukua mzizi wa mti ulio katisha njia
iii.
Chukua tawi la mti unaitwa Ututukanga. Huu mti wa Ututukanga
unapatikana porini na huwa linaonekana shina lake na matawi
yake tu, lakini mzizi wake huwa hauonekani.
iv. Unachukua mti unaitwa Msonihya
v. Unasaga pamoja na mti unaitwa mwavi.
vi.
Baada ya hapo unachukua kuku mweusi, unamfunga kwenye kitambaa
cheusi bila kumchinja, unachukua chungu cheusi, unamuunguza mpaka
anakuwa mkaa, halafu unamsaga pamoja na miti iliyo tajwa hapo
juu, unachanganya na mafuta ya simba.
vii. Unachukua buja ama dulya la ugali wa kilioni
viii.
Kamba ya kitanda alicho lalia maiti, au kama maiti ipo kwenye
nyumba ya nyasi, unachomoa nyasi wakati maiti imo ndani.
ix. Unachimba mzizi wa mti unaitwa mputika bila kivuli chako kugusa mti..
x. Unaunguza vyote kwa pamoja ukiwa na kaniki nyeusi bila kuvaa nguo yoyote usiku wa manane
xi. Unaipika njia panda pamoja na mafuta ya mti mmoja wa porini ambao jina lake linahifadhiwa hapa.
Baada ya hapo, mtu atachanjiwa na kuongeshwa pamoja na kufanyiwa tambiko maalumu.
Basi wachawi watakuwa wakijaribu kutaka kukutupia uchawi, wanakuwa hawakauoni kwenye rada zao za kichawi
SWALI NAMBA TANO : HABARI YAKO DOKTA. NASUMBULIWA SANA NA WIZI NYUMBANI KWANGU. JE IPO NDUMBA YA KUMKAMATA MWIZI ?
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Zipo
ndumba nyingi za kuwakamata wizi. Leo nitataja ndumba rahisi
kabisa ya kumkata mwizi. Ukifanya ndumba hii, basi mwizi
atajileta mwenyewe na kuomba msamaha.
i. Unachukua kinyonga akiwa mzima
ii. Unaponda majani ya kisamvu
iii.Unachukua na changarawe za njiani ambazo, hutembea mvua ikinyesha.
iv.
Huyo kinyonga unamuweka kwenye hayo majani ya kisamvu pamoja na
hizo changarawe, unafunga kwenye kitambaa cheusi halafu unafunga
jikoni, kwenye sehemu inayo toka moshi. Utamuacha hapo kwa muda
wa siku saba.
Baada
ya siku sita, unamtoa hapo kwenye moshi, unasaga ukiwa umefumba
macho halafu unaenda kuvifunga kwenye mti kwa muda wa siku
saba. Kabla siku saba hazijaisha, mwizi wako atarudi mwenyewe. Na
kama mwizi yumo humo humo ndani, atajisalimisha mwenyewe mara
moja.
Hii dawa moja tu, lakini zipo nyingine nyingi.
SWALI
NAMBA SITA : DOKTA NASIKIA WACHAWI WANA UWEZO WA KUTUMIA
UCHAWI KUMSHIKA MWANAUME KIMAPENZI . JE NI KWELI? NA WANAFANYAJE
FANYAJE ?
DOKTA. MUNGWA KABILI ANAJIBU.
Katika masuala ambayo uchawi una ishi na kutawala basi ni suala la mapenzi.
Asilimia
kubwa ya watu wanao enda kwa waganga, huenda huko kwa sababu
ya mapenzi au kwa sababu ya mambo yanayo sababishwa na
mapenzi.
Uchawi
wa mapenzi upo wa aina nyingi sana. Nikisema nianze kutaja na
kuelezea kwa kila aina ya uchawi na ulozi katika mapenzi hapa,
sitamaliza kwa sababu upo uchawi wa aina nyingi sana.
Nitataja
na kuelezea kwa ufupi sana, aina chache za uchawi katika
mapenzi, halafu nitaelezea aina moja ya uchawi wa mapenzi ambao
ni uchawi hatari na wenye nguvu sana.
KUMSHIKA
MWANAUME KATIKA MAPENZI ; Kumshika mwanaume katika mapenzi,
wachawi huchukua njiwa wawili jike dume walio zaliwa kiota kimoja
pamoja na kiota chawe, kisha njiwa hao huchinjwa , hupasuluwa na
mioyo yao hunyofolewa, huchemshwa kwenye mafuta ya mti mmoja
unapatikana porini, halafu husagwa hadi kuwa unga unga. Baada ya
hapo huchukua njugu mawe nyeusi moja, huchanganya na mti unaitwa
mlama, pamoja na miti mingine mitatu ya porini, kisha husagwa
pamoja na ile mizoga ya njiwa.
Vyote
hivi kwa pamoja, huchanganywa na vizimba vitatu vya ndumba za
kichawi, halafu mwanaume huwekewa kwenye chakula, basi mwanaume huyo
atakuwa hasemi chochote kwa mwanamke huyo.Mwanamke atakuwa mama
ake atakuwa baba ake. Ni uchawi mbaya sana huu.
KUMFANYA MWANAUME ASIENDE NJE YA NDOA :
Kumfanya
mwanaume asiende nje ya ndoa, wachawi huchukua kamba ya mbuzi,
moyo wa kondoo, mti unaitwa INAMA NIKUCHUME ( Mti huu
unapatikana Kigoma tu, na watu wa kigoma ndio huuita jina hilo),
mti unaitwa Inyazya kisha vinasagwa kwa pamoja halafu
vinachanganywa na nta ya nyuki, kisha wanatafuta kucha, au nywele,
au ndevu, au uzi wa nguo yake yoyote, halafu vinakaangwa kwa chumvi
ya mawe pamoja na vizimba vya zote \nilizo zitaja hapo juu,
kisha vinafungwa kwenye kitambaa chekundu, halafu vinafukiwa
mlangoni au kwenye mti wowote. Basi mwanaume huyu hawezi kwenda
nje ya ndoa yake.
MWANAUME
AKUONE WEWE TU KILA ANAPOKUWA NA MWANAMKE MWINGINE : Wachawi
hutchukua maji ambayo mwanamke ametumia kunawa uso wake kisha
huchanganya na ndumba 13 za kichawi pamoja na vizimba vyake
kisha kutengeneza ndumba itakayo mfanya mume wa mwanamke huyo
kuwa anaumuona mke wake wakati wote na pia kuwa anaona kama
anatokewa na mke wake kila anapo kuwa na michepuko.
KUMFANYA
MUME AKUPE MSHAHARA WAKE WOTE AU PESA ZAKE ZOTE KILA AKIZIPATA:
Uchawi huu umewalostisha wanaume wengi sana. Hapa mchawi anacho
chukua manii za mwanaume aliye mkusudia, ana changanya pamoja na
baadhi ya vitu alivyo pewa na mwanaume huyo, halafu vinaenda
kutengenezwa kichawi kwa kutumia ndumba za kichawi, basi mwanaume
huyo atakuwa kila akipata mshahara wake anapeleka zote kwa
mwanamke huyo. Asipojistukia mapema, anaweza uza kila kilicho
chake.
KUMVUTA
MPENZI : Ipo miti mitatu inapatikana porini, miti hutumika
kumuita kichawi mwanamke au mwanaume aliye kusudiwa.
KUMTEGA DAWA ZA MAPENZI MWANAMKE AU MWANAUME.
Chaurembo kaenda kwa wachawi, na kuwaomba wampe msaada wa kichawi ili aweze kumteka kimapenzi Ndugu., Maridadi.
Wachawi
watamchukua Chaurembo, watampa ndumba za aina tatu. Ndumba ya
kwanza, atachanjiwa, kichwani na katika pembe zote za mwili wake.
Ndumba ya pili atatumia kunywa, na ndumba ya tatu atatumia
kuoga na kuchoma.
Sikui
tatu baada ya kuanza kutumia ndumba hizo, Chaurembo atamuota
Maridadi anapita katika sehemu ambayo Chaurembo anaifahamu.
Chaurembo atatakiwa kuikariri ndumba hiyo.
Kesho
yake, saa saba mchana, Chaurembo atatkiwa kwenda hadi mahali
alipo muona Maridadi akiwa anapita,akifika katika eneo hilo,
atatakiwa kumwaga dawa aliyo pewa.
Maridadi lazima atapita katika eneo hilo, na akipita tu, basi anakuwa amenasa kwenye penzi la Chaurembo.
Maridadi atamtafuta Chaurembo kwa udi na uvumba na atafanya kila kitu anacho kitaka Chaurembo.
Huu ni uchawi mbaya sana na hutumika hata katika mambo yasiyo ya mapenzi.
SIKU NYINGINE NITAELEZEA KWA UREFU SANA KUHUSU UCHAWI MBALIMBALI UNAO TUMIKA KATIKA MAPENZI.
SWALI NAMBA SABA : JE NI KWELI WACHAWI WANA UWEZO WA KUWAACHANISHA WAPENZI KWA KUTUMIA UCHAWI.
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Ni
kweli kabisa, wachawi wana uwezo wa kuwaachanisha wapenzi. Mke na
mume walio ona kwa sherehe ya mamilioni wanaweza kuachana
ndani ya wiki moja.
Zipo njia nyingi sana wanazo tumia, ila leo nitaitaja moja:
i.Wanachukua mti unaitwa mpuga mbu.
ii. Mkia wa ndege wa porini anaitwa katyente
iii. Picha ya mke na mume walio kusudiwa pamoja na majina yao.
iv. Wanachanganya na vizimba vyake.
v.
Vitu vyote hivyo vinasagwa kwa pamoja, kisha vinakaangwa kwa
kutumia chumvi ya mawe, halafu vinaen da kuchomwa jalalani.
Hata kama wanapendana vipi,wote wataachana.
Ndumba
hii ndio inayo tumika pia kushusha thamani ya cheti cha mtu.
Hata kama amesoma vipi, hawezi kupata kazi kama akifanyiwa
uchawi huu.
Kwa leo naomba niishie hapo, kesho nitaendelea tena na makala haya.
MAKALA
HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI, MTALAAMU ALIYE BOBEA
KATIKA MASUALA YA ULIMWENGU USIO ONEKANA. ANAPATIKANA JIJINI DAR
ES SALAAM, KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.
Reviewed by The Choice
on
9:34:00 PM
Rating:
No comments: