MMILIKI WA MABASI YA NGORIKA AFARIKI DUNIA..AGONGWA NA GARI
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu
Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia
mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati
akizungumza na simu.
Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga
Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku
katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe.
Alisema Mberesero ambae mabasi yake
hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na
singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake
oil na kugongwa na gari hilo.
Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam
Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja
kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta.
Kama unavyojua bosi wetu pamoja na
kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta
mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga
alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanja cha kujenga kituo kipya
cha mafuta,alisema Adam.
Alisema bosi wake huyo alikuwa
ameliweka gari lake katika kituo cha mafuta cha Lake oil na kwamba
alishuka kwajili yakuelekea katika Kiwanja hicho.
Wengi waliokuwepo eneo la ajali hawakujua kama ni yeye hadi tulipokwenda kuchukua mwili wake ndipo wakashtuka,Alisema.
Kamanda Mihayo alisema wanamsaka Dereva aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe na kusababisha kifo.
MMILIKI WA MABASI YA NGORIKA AFARIKI DUNIA..AGONGWA NA GARI
Reviewed by The Choice
on
9:17:00 PM
Rating:
No comments: