SITI ZA UWANJA WA BESIKTAS UTURUKI ZAFUNGWA SCREEN KILA KITI... MECHI INACHEZWA UNASHUHUDIA KWENYE SITI
Baada
ya siku 1065 za kusubiri ukarabati wa uwanja wao, wakiwa ‘wanadoea’
viwanja vingine mashabiki wa Besiktas wamerejea kwenye Uwanja wao wa
Vodefone Arena.
Uwanja
mpya, safi pembezoni mwa jiji la Istanbul, tena uwanja huo wenye uwezo
wa kuchukua mashabiki 43,000. Jukwaa lake moja, situ zake hazipatikani
uwanja wowote duniani.
Katika
kila siti katika jukwaa hilo, shabiki anakuwa anaona pia kupitia TV
iliyo mbele yake, yaani nyuma ya siti ya mbele yake kama inavyokuwa
kwenye ndege au mabasi ya kisasa.
Ana nafasi ya kuangalia mechi au marudio ya slow motion kwa karibu zaidi. Hiyo ndiyo kazi ya Waturuki.
Nchini humo, timu kubwa zaidi ni Galatasaray, inafuatiwa na wapinzani wao wakubwa Fenerbahce halafu Besiktas.
SITI ZA UWANJA WA BESIKTAS UTURUKI ZAFUNGWA SCREEN KILA KITI... MECHI INACHEZWA UNASHUHUDIA KWENYE SITI
Reviewed by The Choice
on
8:32:00 PM
Rating:
No comments: