Rammy Gallis Achukia Kuitwa Kanumba Feki

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu, kama ilivyo kawaida yetu ni kukupa wewe msomaji kitu roho inapenda kwa kuwa tunajua unapenda kujua maisha halisi ya mastaa wetu wa hapa Bongo.
Leo aliyetupendezeshea ukurasa wetu ni muigizaji anayefananishwa na marehemu Steven Kanumba, Rammy Gallis anayeishi maeneo ya Chang’ombe jijini Dar.
Ili kujua maisha yake halisi, twende pamoja chini:
RAMMY GALLIS
Rammy Gallis
Anapenda kufanya NINI akiamka asubuhi?
“Kitu cha kwanza kabisa napenda kufanya usafi wa mwili wangu na kukiweka kitanda nilicholalia katika hali ya usafi na kufanya mazoezi kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kuendelea na vitu vingine.”
Anapenda kufungua kinywa na nini? Mlo wa mchana je?
“Mara nyingi chai siyo mpenzi sana lakini kama nitakunywa napendelea iliyo na tangawizi ikiwa bila kitafunwa, mchana napenda kula chakula chochote kizuri kama wali nyama au ugali.”
Anapikiwa na nani?
“Mara nyingi napika mwenyewe ila nikitembelewa na ndugu zangu wa kike hunisaidia.”
Anapenda kufanya nini akiwa nyumbani?
“Napenda sana utulivu ambapo huwa najifungia ndani nikiangalia runinga na kusikiliza muziki.”
Vipi kuhusu kazi ndogondogo za nyumbani?
“Mimi sijivungi kila kazi nafanya mwenyewe kama kuosha vyombo na usafi wa nyumba kwa ujumla, sipendi kusubiria mtu aje anifanyie wakati uwezo ninao.”
Nini unachokichukia?
“Sipendi ukorofi na pia sipendezwi na mtu kuniudhi napenda sana kuwa na amani ya hali ya juu na sihitaji kumsonenesha mtu kwa njia yoyote ile.”
Anatarajia KUOA lini?
“(Kicheko) bado kidogo ila ninaye nimpendaye kwa dhati kabisa tuombe Mungu niweze kumuoa huyo.”
Anamzungumziaje Kanumba na kufanana kwao?
“Ni kweli tunafanana kidogo lakini namkumbuka kwa kazi zake nzuri ila kuna watu wananikorofisha kwa kuniita Kanumba feki, mimi na yeye tulikuwa tukifanana kidogo tu na inawezekana uwezo wa kazi zetu ni tofauti ila nitaendelea kumheshimu siku zote.”
Chanzo:GPL
Rammy Gallis Achukia Kuitwa Kanumba Feki Rammy Gallis Achukia Kuitwa Kanumba Feki Reviewed by The Choice on 1:41:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.