WAFANYA KAZI WENYE ELIMU YA Darasa la Saba waiponza TTCL, ATCL yaligharimu Taifa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) limebainika kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wenye elimu ya darassa la saba wanaolipwa mishahara kwa muda mrefu huku utendaji wao uyaangamiza na kulitia Taifa hasara kulingana na elimu waliyonayo.
Kadhalika, Shirika la Ndenge Tanzania (ATCL) limebainika kuwa moja kati ya mashirika yanayolitia hasara Taifa kutokana na kutumia gharama kubwa kulipa rundo la wafanyakazi wasiokuwa na majukumu katika Shirika hilo.
Hayo yamebainishwa juzi na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad alipokuwa akitoa mafunzo kwa wabunge wanaounda kamati nne za Bunge kuhusu mambo ambayo wanapaswa kuhoji wanapokuwa kwenye vikao vya bajeti.
Alisema kuwa TTCL na ATCL wameendelea kuwalipa wafanyakazi hao mishahara kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi hadi sasa wakati elimu yao ya darasa la saba wakati hakuna kazi wanazofanya kuzalisha na kuendeleza taasisi hizo za umma.
“TTCL halina faida yoyote kwenye nchi hii kwa zaidi ya miaka kumi sasa, watu wanalipwa mishahara lakini hakuna kinachofanyika. Ukienda pale asilimia kubwa ya wafanyakazi ni darasa la saba,” alisema Profesa Assad.
Profesa Assad alipendekeza mashirika hayo kufutwa ikiwa yanaendelea na uzalishaji huo kwani yanalitia hasara taifa kwa kutumia rasilimali nyingi kuliko wanachozalisha.
Akiizungumzia ATCL, alisema shirika hilo linaingizia taifa hasara kwakuwa na wafanyakazi 300 wakati ina ndege mbili tu hivyo hakuna mapato ya kodi yanayopatikana kulinganisha na gharama za uendeshaji.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa Kamati za Bunge walieleza kuwa mara kadhaa wanapozihoji taasisi hizo huambiwa kuwa chanzo cha changamoto hizo ni kupewa bajeti ndogo na serikali.
“Tumejaribu kuhoji juu ya mashirika haya likiwemo la ATC, wanadai bajeti wanazopewa na Serikali kwa ajili ya kuendesha mashirika hayo zinakuwa hazikidhi mahitaji halisi na haziji kwa wakati hivyo hushindwa kujiendesha,” alisema Mbunge wa viti maalum, Raisa Abadallah Mussa (CUF).
WAFANYA KAZI WENYE ELIMU YA Darasa la Saba waiponza TTCL, ATCL yaligharimu Taifa
Reviewed by The Choice
on
9:20:00 PM
Rating:
No comments: