Nilisingiziwa Mtoto Anafanana na Diamond – Idris

Mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa alipotoka kwenye mashindano ya Big Brother Africa alipotua nchini Tanzania alisingiziwa kuwa na watoto watatu na mwanamke mmoja wa Mtwara alimleta mpaka mtoto mwenyewe kwake.
idriss12

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Mkasi’ kinachorushwa na EATV Idris Sultan alisema alivyoletewa mtoto alibaki akishangaa na alivyomwangalia vizuri yule mtoto aliona ni kama anafanana na msanii Diamond Platnumz kwanza kutokana na rangi yake na jinsi yule mtoto alivyo.
“Unajua siku nimerudi kutoka kwenye mashindano ya Big Brother nilisingiziwa kuwa nina watoto watatu, na mmoja alimleta mtoto mpaka nyumbani lakini nilivyomuangalia yule mtoto niliona kama anafanana na Diamond Platnumz kwanza ile rangi ya weusi na jinsi mtoto alivyo, nikaona isiwe taabu nikampigia simu Diamond Platnumz nikamwambia na yeye akaja kumuangalia yule mtoto lakini akasema na yeye si wake. Yule mama mtoto alikuwa anatokea Mtwara hivyo mpaka leo baba wa yule mtoto bado hajafahamika” alisema Idris Sultan
Mbali na hilo mchekeshaji huyo ameelezea namna ambavyo anaweza kuishi na marafiki zake wa karibu ambao kwa sasa wote hawaongea, akiwepo Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na Wema Sepetu na ndipo aliposema yeye anaweza kwenda nao sawa.
“Unajua mimi ninapokuwa na Wema Sepetu ninazungumza naye mambo yangu mimi na yeye hivyo siwezi kuwa na yeye nianze kuzungumza mambo ya mtu mwingine na hiyo ndiyo njia inayofanya niweze kuishi nao pasipokuwa na tatizo, unajua hawa wote kwangu mimi ni muhimu sana mimi nawahitaji wao na sijui kama wao wanatambua hilo” alisisitiza Idris Sultan
eatv.tv
Nilisingiziwa Mtoto Anafanana na Diamond – Idris Nilisingiziwa Mtoto Anafanana na Diamond – Idris Reviewed by The Choice on 8:29:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.