RC Makonda: Ni marufuku kuwasaidia Ombaomba barabarani jijini Dar


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dar es salaam Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dar  wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua
RC Makonda: Ni marufuku kuwasaidia Ombaomba barabarani jijini Dar RC Makonda: Ni marufuku kuwasaidia Ombaomba barabarani jijini Dar Reviewed by The Choice on 6:27:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.