Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China
Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi
Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.
Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.
Wakuu
hao wa wilaya na wakurugenzi wao walikuwa
waondoke jana kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, lakini habari
zinaarifu kuwa Ikulu iliamua kutotoa kibali, hali
inayozidisha ubashiri kuwa uamuzi huo umetokana na kukamilika kwa uteuzi
wa wakuu wapya.
Safari hiyo ilishakamilika kwa kiwango kikubwa
baada ya kupata visa na wengi wao kuwasili jijini Dar es Salaam tayari
kwa safari hiyo, lakini wakalazimika kurejea kwenye vituo vyao baada ya
kukosa kibali cha Ikulu ambacho hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi.
Mara
tu baada ya kuapishwa Novemba 5 mwaka jana, Rais John Magufuli
alitangaza kudhibiti safari za nje za watumishi na viongozi wa umma kwa
kuagiza kuwa Ikulu ndiyo itakayotoa kibali baada ya kujiridhisha na
umuhimu wa safari hizo kwa Taifa.
Tangu atoe agizo hilo, ni
mawaziri wawili tu ambao wameruhusiwa kwenda Vietnam kwenda kujifunza
kilimo na viwanda. Mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo,
Mifugo na Uvuvi) na Charles Mwijage (Viwanda na Biashara).
Naibu
Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alikwenda nchini Ethiopia kuhudhuria
mkutano wa mawaziri wa fedha, wakati kwa nyakati tofauti Makamu wa Rais
Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikwenda Afrika Kusini na
Botswana.
Mpaka sasa, Rais Magufuli amefanya safari moja tu ya nje alipokwenda Rwanda kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari.
Lakini
safari ya wakuu hao wa wilaya ilikuwa ifadhiliwe na China, kwa mujibu
wa habari hizo na hivyo isingeisababishia Serikali kutumia vibaya fedha
za walipa kodi.
Uamuzi huo unaonekana kuzingatia zaidi uteuzi wa
wakuu wapya ambao taarifa zinasema unaweza kutangazwa wakati wowote
kuanzia sasa, wakati wa wakurugenzi wa wilaya unatazamiwa kutangazwa
baadaye wiki hii au wiki ijayo.
Alipoulizwa kuhusu suala
hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene
alikiri kuwapo kwa safari hiyo, lakini akasema hajui kama imeidhinishwa
na Ikulu kwa kuwa si muhusika.
“Katika hatua za awali nilisaini
safari hiyo kuwaruhusu waende China, lakini sijui kama wamenyimwa kibali
kwa sababu hilo si suala la ofisi yangu,” alisema Waziri Simbachawene.
Kama
ni kweli, alifafanua Simbachawene, inaweza kuwa ni kutokana na umuhimu
wao wa kuwatumikia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. “Hawawezi kuondoka
na kuziacha wilaya zao ilhali wao ndiyo waangalizi,” alisema Simbachawene.
Akiwa
Chato mkoani Geita, Rais aliwataka wakuu wa wilaya kuchapa kazi badala
ya kuwa na woga wa kutoteuliwa akisema uchapaji kazi ndio utawafanya
waendelee kuwapo kwenye nafasi zao.
Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China
Reviewed by The Choice
on
6:26:00 AM
Rating:
No comments: