ALIYEWAAMBUKIZA 200 NA HIV AFUNGWA MIAKA 25
Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.
Daktari huyo bandia
alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya
ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.
Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Yem Chrin alikuwa
akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji
cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.
Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.
Kesi hiyo imefichua
uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika
maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.
Utafiti umebaini kuwa
zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari
bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa
ALIYEWAAMBUKIZA 200 NA HIV AFUNGWA MIAKA 25
Reviewed by The Choice
on
6:28:00 AM
Rating:
No comments: