MAMA YAKE DIAMOND AFANYA KUFURU HII
Mama Diamond akifanya usafi kwenye nyumba yake ya Tandale hivi karibuni.
Mama
wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
Sanura Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake kwa kununua
mtaa mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba yake
aliyokuwa akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi milioni 100.
Diamond na Mama yake Sandra.
Chanzo
chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo
ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’
huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia
ujenzi sambamba na binti yake, Esma.
Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.
“Mama
Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia
ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe
wao,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo
hicho kimezidi kutiririka kuwa mama Diamond anataka kuifanya nyumba
hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na kuiboresha, kuna mpango wa
kutengenezwa swimming pool (bwana la kuogelea).
Ikiwa inakarabatiwa.
Mara
baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba hiyo
na kuzungumza na mama Diamond aliyekuwa bize kusimamia ujenzi.
Baada ya kukarabatiwa.
“Jamani!
Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu iwe
bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda mje
mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio
nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.
MAMA YAKE DIAMOND AFANYA KUFURU HII
Reviewed by The Choice
on
11:43:00 PM
Rating:
Safi bimkubwa tumia matunda yako uliyoyapanda wewe pamoja na mama yangu ndo malkia wangu,ynajua jinsi gani ya kutumia fursa big up Bi sandara
ReplyDelete