STAR ALIKIBA AMFUNGUKIA MAZITO JOKATE, NA KUMBWAGA AZARANI
DAR ES SALAAM: Staa
anayesumbua na wimbo wa Lupela, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa
kumlipua Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa kusema hakuwahi kuwa na mpango wa
kudumu naye penzini, Risasi Jumamosi linakupa ubuyu kamili.
Hivi karibuni, Jokate
alizungumza na wanahabari wa Global Publishers na kudai amemchoka mpenzi
wake huyo hivyo ameamua kumuacha rasmi Kiba ambapo habari hiyo
ilichapwa jana kwenye Gazeti la Ijumaa.
kiba jokateKiba na Jokate.
Chanzo kilicho karibu na
Kiba kimeweka bayana kuwa mkali huyo hakuwa na mpango na penzi la Jokate
lakini alilazimika kuwa naye karibu kwa shughuli za kikazi (muziki).
“Tunamshangaa Jokate kusema
eti amemchoka Kiba leo wakati anajua kitambo tu Kiba hakuwa na mpango
naye. Kiba alilazimika ‘ku-fake’ penzi kwa sababu walikuwa wanafanya
kazi za pamoja, hakuwa na jinsi.
Jokate
“Jokate mwenyewe anajua
kwamba Kiba hakuwa na mpango naye. Nafikiri kajitokeza kwenye ‘media’
ili aonekane yeye ndiyo kamuacha Kiba kumbe mwenzake hata hakuwa na
mpango wa kuwa naye,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta
Kiba katika simu yake ambapo alidai hapendi sana kuanika mambo yake
binafsi kwenye vyombo vya habari lakini mmoja wa mameneja wake aliyeomba
hifadhi ya jina, alifafanua suala hilo.
“Kiba hakuwa na mpango na
Jokate na ndiyo maana kila siku tunapokuwa kwenye kazi zetu hapendi
umtajie ishu za Jokate hata kidogo na alikuwa akisisitiza kweli lakini
sisi tulikuwa tunalazimisha waendelee kwa sababu tulikuwa tunafanya kazi
za pamoja,” alisema meneja
STAR ALIKIBA AMFUNGUKIA MAZITO JOKATE, NA KUMBWAGA AZARANI
Reviewed by The Choice
on
11:44:00 PM
Rating:

No comments: