KISA URAIA WA UGANDA WASABABISHA Dr Wangwe Ambaye Aliteuliwa Kukaimu NSSF na Kisha 'Kutumbuliwa' ndani ya Masaa Matano
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)
imetetea uraia wa Dk Carina Wangwe ikisema ni Mtanzania kwa kuandikishwa
tangu mwaka 1999.
Dk Wangwe aliteuliwa juzi na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kudumu katika nafasi hiyo
kwa saa tano kabla ya uteuzi huo kutenguliwa kwa maelezo kuwa taratibu
hazikuwa zimekamilika.
Kutenguliwa huko kulielezwa na baadhi ya
watu kuwa ilikuwa ni kwa sababu mkuu huyo wa Tehama SSRA ni raia wa
Uganda, madai ambayo yalikanushwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue,.
Taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa jana usiku na Kitengo
cha Mawasiliano cha SSRA, ilisema Dk Wangwe aliandikishwa kuwa raia
baada ya kukidhi vigezo vya kuasiliwa (naturalisation) kwa mujibu wa
kifungu cha 11 cha Sheria ya Uraia Na. 6 ya mwaka 1995.
Sambamba
na hilo, taarifa hiyo ilisema Dk Wangwe aliukana uraia wa Uganda ikiwa
ni pamoja na kurudisha pasipoti ya nchi hiyo aliyokuwa akiimiliki.
“Hivyo
amekuwa raia wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 na anamiliki cheti
cha uraia Na. 58391 kilichotolewa na mamlaka husika tarehe 23 Aprili,
1999,” inasomeka taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inasema Dk Wangwe ni
mtumishi halali wa SSRA kuanzia mwaka 2011 hadi sasa baada ya kukidhi
vigezo vya uraia na utaalamu.
“Ana uzoefu wa miaka 21
akiitumikia Tanzania katika nyadhifa tofauti ikijumuisha Chuo Kikuu
Kishiriki cha Ardhi (miaka mitatu), Mfuko wa Pensheni wa PPF (miaka 9)
na SSRA,” inasema taarifa hiyo.
KISA URAIA WA UGANDA WASABABISHA Dr Wangwe Ambaye Aliteuliwa Kukaimu NSSF na Kisha 'Kutumbuliwa' ndani ya Masaa Matano
Reviewed by The Choice
on
1:03:00 PM
Rating:
No comments: