MREMBO KIM KARDASHIAN ANATAKA MUME WAKE KANYE WEST APATE MSAADA WA KITALAAM
Kim Kardashian anamtaka mume wake Kanye West apate msaada wa kitaalam, kwa mujibu wa ripoti ya US Weekly.
Kim
amefedheheshwa na tabia ya hivi karibuni ya mume wake ikiwemo diss yake
ya Taylor Swift kwenye album ya The Life Of Pablo na kumuomba msaada wa
kifedha, mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg.
Chanzo
kilicho karibu na familia yao kimedai kuwa Kim ana wasiwasi na tabia
yake mume wake na wamekuwa na matatizo makubwa yanayokua kila siku.
Pamoja
na Kim kumtaka mumewe ajirekebishe, rapper huyo bado ameendelea
kuitumia Twitter kutoa malalamiko yake. Mapema mwezi huu iliripotiwa
kuwa Kim amekuwa akichukizwa na kile mumewe anachopost kwenye Twitter.
Jumatano hii pia Kanye alilianzisha kwa kuwashambulia waandaji wa tuzo za Grammy.
CHANZO na Bongo5.
MREMBO KIM KARDASHIAN ANATAKA MUME WAKE KANYE WEST APATE MSAADA WA KITALAAM
Reviewed by The Choice
on
6:52:00 AM
Rating:
No comments: