RAY C ASEMA KWASASA BORA ATOKE NA MSUKUMA MKOKOTENI KULIKO MSANII
Msanii
wa muziki Ray C amedai hawezi toka kimapenzi tena na msanii kutokana na
kuumizwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Lord Eyes.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha
ENewz cha East Africa Television kuwa toka aachane na Lord Eyes hajawahi
kuingia tena kwenye mahusiano na kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana
mpaka yeye kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kipindi hicho.
“Kwa sasa bado sina boy friend, now
nina marafiki tu kiukweli nafasi hiyo bado maana Lord Eyes aliniumiza
sana, nilimpenda sana na ndiyo maana nilifanya alichokuwa akifanya,
sikutegemea kama ingekuwa vile, hata kwenye drugs unakutana na rafiki
yako anafanya hiki na wewe utataka kufanya ili aone upo naye pamoja, ila
kwa sasa mimi na wasanii hapana, ni bora hata nitoke na msukuma
mkokoteni ili mradi anipende maana mimi nina mapenzi ya kweli ndiyo
maana unaona hata nyimbo zangu nyingi ni za mapenzi” Alisema Ray C.
RAY C ASEMA KWASASA BORA ATOKE NA MSUKUMA MKOKOTENI KULIKO MSANII
Reviewed by The Choice
on
6:53:00 AM
Rating:
No comments: