BREAKING NEWZZZ...Waziri Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro

NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora,Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro kutoka na uzembe uliipelekea hasara serikali ya bilioni 1.
Vilevile Waziri Kairuki amewasimamisha pia mkuu wa chuo hicho tawi la Dar es salaam,Joseph Mbwilo na Silvanus Ngata ambaye naye ni mkuu wa chuo hicho tawi la Tabora,
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu,Jijini Dar es Salaam,Waziri Kairuki amesema amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watu hao ni baada ya kubaini kuwepo na uendaji usio ridhisha katika vyuo hivyo,
Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika chuo hicho na pia kuwa na usimamizi usio na ufanisi,
Amesema kuwa uzembe huo uliofanywa na Nassoro umepelekea hadi matawi ya vyuo hivyo kuathirika .
“Mwaka 2011 hadi 2013 bwana Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo cha Mtwara tofauti na ile fedha iliyopangwa,na hata ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ilithitisha ubadilifu huo ,
“Lakini huyo Nassoro baada ya kugundua kosa hilo alimwamisha bwana Ngata na kumpeleka tawi la chuo cha Tabora na kuendelea na wazifa wake na huyo bwana Ngata kutokana na haya hakufuta taratibu pia namsimisha kazi”amesema Waziri Kairuki,
Pia waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo,
“Huyu Mbwiro kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi za kiasi cha bilioni 1 kwa mwaka fedha mwaka 2014,lakini licha ya ubadilifu huyo,huyo Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa fedha,kwahiyo huyo bwana Mbwiro namsimiasha pia,”amesema Waziri Kairuki,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati Waziri Kairuki anawasimamisha watendaji hao,mmoja wa watendaji hao,Nassoro alikuwepo kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea,mara baada ya waziri Kairuki kutaja kumsimamisha kazi,alionekana kama mtu mwenye kupata na mshangao huo akijizuia hali yake isionekane.
BREAKING NEWZZZ...Waziri Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro BREAKING NEWZZZ...Waziri Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro Reviewed by The Choice on 2:02:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.