Meya Kinondoni amwambia DC Makonda Asiingilie kazi zisizo Muhusu.



Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amemuonya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuacha tabia ya kuingilia majukumu ya Halmashauri, badala yake afanye kazi zinazomuhusu.
Pia alisema uingiliaji huo ni utapeli uliomsababisha Rais John Magufuli kuagiza kila waziri akatwe Sh. milioni moja katika mshahara wake, pamoja na yeye mwenyewe, Waziri Mkuu Kassim Majalaliwa na Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na shule mpya katika Jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli alifikia uamuzi huo alipokuwa akizungumza na Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa Dar es Salaam, baada ya kuelezwa matatizo ya ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza katika mkoa huo, lililotokana na utekelezaji wa ahadi ya elimu bure.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meya Jacob (Chadema) alisema ameradhimika kumuonya DC Makonda kutokana na tabia ya kutafuta sifa ili aonekane mchapakazi, hali ya kuwa ana dandia kazi zisizomuhusu.
Alisema hakuna sheria inayomruhusu Makonda kushirikiana kikazi na Halmashauri hadi awasilishe barua ya maombi kwa Mkurugenzi ama Meya kama anahitaji kufanya jambo lolote.
Majukumu
Jacob alisema ma-DC nchini wana majukumu muhimu matatu tu, ikiwemo Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Uenyekiti wa Kamati za Mashirikiano pamoja na kuwa Kiunganishi wa Serikali ya Mtaa na Serikali Kuuu.
Kuhusu wenye uwezo wa kuzungumzia maswala ya Halmashauri, Jacob alisema ni watu watatu wenye mamlaka ambao ni Mkurugenzi, Meya na Afisa Habari lakini si DC kwa kuwa haimuhusu.
“Kitu kilichosababisha nieleze haya na kutoa ufafanuzi huu ni kutokana na kitendo alichokifanya Makonda hivi karibuni kuueleza umma kwamba Halmshauri ya Kinondoni imepokea USD 300 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara hali ya kuwa hakupaswa kulizungumzia kwani lipo nje ya uwezo wake,
Ilikuwa bado ni taarifa ya siri lakini akaidukua na kukurupuka kuitangaza, jambo ambalo limesbabisha mtafaruku mkubwa kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wakihoji kwanini taarifa hizo zitolewe bila ya kamati kupitisha,’alisema.
Jacob alisema kutokana na hatua hiyo, wanamtaka Makonda kutoingilia majukumu yasiyokuwa yake;
“DC hana uwezo wa kupanga bajeti wala kutoa fidia ama kuzungumzia kitu chochote kinachosu Halmshauri hadi aombe ruhusa, pia hakuna mahusiano yoyote baina ya DC huyo na Halmashauri,”alisema
Pia alisema walimvumilia DC kutokana na vitendo vyake lakini kwa sasa wamefikia mwisho na wanamuonya kuacha tabia za udukuzi.
Utapeli
Kuhusu utapeli huo wa Makonda kwa Rais Magufuli alisema kuwa Halmashauri hiyo haina shida ya msaada wowote kutoka kwenye mshahara wa rais.
Alisema halmshauri hiyo inakusanya takribani sh.bilioni 46 kwa mwaka, huku ikipata kiasi cha sh.bilioni 78 ikijumuiha na mishahara ya watumishi, ambapo kwa mwaka inapata sh.bilioni 152.
“Hatukupenda rais atangaze kukata mshahara wake kwa kuwa hatuna shida nao, kama ingekuwa uwezo wetu tungeamuandikia barua asikate bali uende kusaidia Halmashauri ya Ilala na Temeke lakisi sio kwetu,”alisema.
Alieleza kuwa hatua hiyo inatokana na halmashauri hiyo kuwa na pato kubwa isipokuwa lilikwamishwa na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), uliopita kwa kufanta ubadhirifu wa fedha.
“Mathalani kuna kigogo wa CCM alikuwa anafanya kufuru kwenye ulipaji kodi wa mabango madogo, ambapo tukikusanya kodi zote za mabango kama inavyotakiwa tunapata zaidi y ash.bilioni 10 kwa mwaka,
Ni aibu kuona DC anahangaika na maombi ya msaada kama omba omba hali ya kuwa Halmashauri ina uwezo mkubwa, alitakiwa aje kutuomba ili tumsaidie lakini sio kukimbilia udukuzi ili aonekane anafanyakazi kubwa,”alisema.
Hofu
Jacob alisema kutokana na udukuzi wa Makonda kuhusu taarifa za utekelezaji wa mradi huo, kwa sasa wajumbe wa Kamati ya Fedha wana hofu dhidi ya Baraza la Madiwani kwa kuwa taarifa zimevuja kabla ya kukaliwa kwa vikao halalali.
Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Halmashauri namba 8 ya mwaka 1982 hairuhusiwi mtu yoyote akiwemo Meya na Mkurugenzi kuzungumzia suala la vikao vya halmashauri nje ya vikao, lakini Makonda amediriki kufanya hivyo.
“Siku zote Mgema akisifiwa Pombe huitia maji, ndio haya anayoyafanya Makonda baada ya kusifiwa na rais kila kazi anajiona anaweza kuifanya ili apate sifa wakati anashindwa kujua baadhi ya vitu si jukumu lake wala havimuhusu,’alisema.
Alisema taarifa za mradi huo (DMDP) zilizosambazwa na Makonda hazikupangwa kwa Kinondoni pekee bali ni mradi uliolilenga jiji la Dar es Salaam, kuwa kama miji mingine mikubwa Duniani ikiwemo Paris Ufaransa, ambapo kuzungumziwa tangu mwaka 2014.
Pia alisema Manispaa imeingiwa na mtanziko kwani Kamati ya Baraza limeanza kuhoji uhalali wa Makonda kuhusu udukuzi huo, hivyo kuna uwezekano wa kupingwa kwa matumizi ya fedha hizo kwenye vikao vya baraza.
“Pia ameibua hofu kwa wananchi wa Bonde la Mto Ng’ombe kwamba watavunjiwa nyumba, hali ya kuwa halmashauri ilishaweka utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi hao takribani sh.bilioni 1.7, huku waliokuwa pembezoni mwa barabara zitakazopitiwa na mradi huo watalipwa sh. bilioni 14,”alisema.
Shule
Kuhusu ujenzi wa Shule za Sekondari ambapo Makonda alitangaza arambee ya uchangiaji Saruji, Jacob alisema anachofanya Makonda ni uongo kwa kuwa sio mjumbe wa Baraza la Madiwani kwani hakupaswa kulizungumzia.
“Tangu apokee mifuko ya Saruji hadi sasa hakuna hata mmoja uliopelekwa kwenye shule, anacofanya ni utapeli tu inatakiwa tujiulize kaipeleka wapi labda iwe kwenye ofisi za CCM,”ALISEMA.
Pia alisema Makonda hana uwezo wa kumfukuza hata mfanyakazi wa kufagia katika ofisi za Halmashauri, wala kubanga bajerti ya sh.5000 au kumuwajibisha mtu yoyote kwa kuwa sio ujukumu lake kiutawala wala kisheria.
Hatua
Jacob alibainisha kuwa kutokana na kumuonya mara kadhaa DC huyo endapo akiendelea kufanya udukuzi basi watawaondoa Maafisa tarafa kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ambao wamekuwa viunganishi wake,
“Kwa kuwa mihimili hii ni tofauti siwezi kumpigia simu Makonda kumuuliza kwanini amezungumzia hayo bali anatakiwa anitafute baada ya kusikia nimeongea haya,’alisema
Meya Kinondoni amwambia DC Makonda Asiingilie kazi zisizo Muhusu. Meya Kinondoni amwambia DC Makonda Asiingilie kazi zisizo Muhusu. Reviewed by The Choice on 1:59:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.