MTANGAZAJI GARDNER G HABASH KUANZA KUSIKIKA LEO CLOUDS FM
Msimu Mpya Clouds FM
Mwezi huu umekuwa wa mapambano makubwa kati ya vituo vya redio viwili jijini Dar es Salaam, Clouds FM na EFM.
EFM walibomoa kipindi
cha Power Breakfast kwa kuwachukua Gerald Hando, Paul James na
mtayarishaji wa kipindi hicho, Abel Onesmo huku Clouds FM wakikibomoa
kipindi cha Ubaoni cha EFM kwa kumchukua mtangazaji wake wa zamani,
Gardener G Habash.
Gardener aka Captain
anaanza kazi rasmi Jumatatu hii kwenye msimu mpya wa kituo hicho kwa
kuendelea kukiendesha kipindi chake cha zamani, Jahazi.
Mtangazaji huyo anadaiwa
kupewa mshahara mnono unaoweza kumfanya kuwa mtangazaji anayelipwa
fedha nyingi zaidi kuliko wote Tanzania. Kwanza miongoni mwa vitu
alivyopewa ili kurejea tena CMG ni gari aina ya Land Rover Discovery na
mashavu mengine mengi.
Kwa upande wa EFM kuna
kila dalili kuwa kipindi hao cha asubuhi kitapata nguvu mpya kuanzia
wiki hii. Haijulikani ni watu wapi Clouds FM wamewachukua kuziba pengo
lililoachwa kwenye Power Breakfast.
MTANGAZAJI GARDNER G HABASH KUANZA KUSIKIKA LEO CLOUDS FM
Reviewed by The Choice
on
3:54:00 PM
Rating:
No comments: