HAYA NDO MANENO YA KWANZA YA MAMA ANNE KILANGO BAADA YA KUTUMBULIWA JIPU NA RAIS MAGUFULI



Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo.


Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.

Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
HAYA NDO MANENO YA KWANZA YA MAMA ANNE KILANGO BAADA YA KUTUMBULIWA JIPU NA RAIS MAGUFULI HAYA NDO MANENO YA KWANZA YA MAMA ANNE KILANGO BAADA YA  KUTUMBULIWA JIPU NA RAIS MAGUFULI Reviewed by The Choice on 9:24:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.