Mbwana Samatta atupia tena, timu yake ikiibuka na ushindi wa 2-1


Timu anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta ya Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Zulte-Waregem katika ligi ya nchini Ubelgiji.

Katika mchezo huo, Mbwana Samatta aliweza kupachika bao kupitia dakika ya 8 ya mchezo huo ya kipindi cha kwanza. Mbali na Mbwana Samatta pia mchezo wa timu hiyo ya Genk Marvin Baudry alifanikiwa kupachika bao la pili dakika ya 15 na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Hata hivyo wapinzani hao wa akina Mbwana Samatta walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi katika dakikaya 45, kwa njia ya penati iliyofungwa na Mbaye Leye.

Mbwana Samatta atupia tena, timu yake ikiibuka na ushindi wa 2-1 Mbwana Samatta atupia tena, timu yake ikiibuka na ushindi wa 2-1 Reviewed by The Choice on 10:26:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.