Majambazi Yaua Wanne na Kupora Supermarket
Wakazi wanne wa jijini Tanga wamekufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa kwa risasi na majambazi .
Majambazi
hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG , walivamia juzi duka kuu
(supermarket) la mfanyabiashara Hamoud Ali lililopo Mtaa wa Swahili
katika kata ya Central jijini Tanga .
Waliokufa
katika tukio hilo ni Ahmed John, Vitus Manfred ambaye ni dereva wa gari
la Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Athumani Seya pamoja na Ali Mpemba
ambaye ni mfanyakazi kwenye duka hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paul tukio hilo ni la juzi saa 1.30 usiku.
‘’Wakati
biashara inaendelea ndani ya hilo duka kuu , ghafla waliingia watu
wengine zaidi kama wateja ambao baada ya muda mfupi walibadilika na
kutoa silaha za moto”, alisema.
Aliongeza
“Kitendo chao hicho kilienda sambamba na amri ya kuwataka watu wote
waliokuwa humo dukani kulala chini ambapo inadaiwa walitii na kisha
wakaamua kuwapiga risasi maeneo ya kichwani wateja wanne waliokuwemo.”
Majambazi Yaua Wanne na Kupora Supermarket
Reviewed by The Choice
on
7:43:00 AM
Rating:
No comments: