KUHUSU SAKATA LA WALIMU KUANZA KUVAA SARE,WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI HUU..!!
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imekanusha taarifa
inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Waziri wake Profesa Joyce
Ndalichako ametaka walimu kuandaliwa sare.
Taarifa iliyotolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema kuwa
taarifa hizo si za kweli na kuwaonya watu wanaotoa taarifa za uzushi
kuacha mara moja. Imesema imejipanga kuhakikisha inachukua hatua za
kisheria kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.
“Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizi si za kweli. Watu
wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili
kuepusha usumbufu unaojitokeza,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa
zilizokuwa zimeenea kwenye mitandao zinasema kuwa Profesa Ndalichako
amesema nguo kwa ajili ya walimu zinaandaliwa ambazo zitakuwa aina tatu.
KUHUSU SAKATA LA WALIMU KUANZA KUVAA SARE,WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI HUU..!!
Reviewed by The Choice
on
6:29:00 AM
Rating:
No comments: