KAMPUNI YA SIMU YA BLACKBERRY KUZINDUZ SIMU ZENYE MFUMO WA ANDROID
Kampuni ya simu ya Blackberry imejipanga kuhakikisha mwaka huu wanazindua simu aina mbili zilizo katika mfumo wa Android.
Akizungumza
na mtandao wa habari wa Falme za Kiarabu (UAE), Mkurugenzi Mtendaji wa
Blackberry, John Chen amesema kampuni yake inataraji kuzindua simu aina
mbili moja ikiwa katika mfumo wa kawaida ikiwa na batani na nyingine
ikiwa ya kugusa kioo (touch screen).
Chen
amesema simu hizo za mfumo wa Adroid zitakuwa za kwanza kutoka kampuni
hiyo baada ya wateja wengi kulalamika kuhusu gharama za kununua simu zao
na simu hizo zitakuwa na gharama ambazo zitawavutiwa wateja wa bidhaa
zao.
“Wateja
wetu wengi wamekuwa wakitwambia kuwa wanataka kununua bidhaa zetu
lakini Dolla 700 ni kubwa kwa simu kama Blackberry Priv na wanavutiwa
zaidi na simu zinazoanzia Dolla 400,” alisema Chen.
KAMPUNI YA SIMU YA BLACKBERRY KUZINDUZ SIMU ZENYE MFUMO WA ANDROID
Reviewed by The Choice
on
7:41:00 AM
Rating:
No comments: