HII NDO MISHAHARA YA RAIS MAGUFULI NA KIKWETE..YAWEKWA WAZI RASMI
OFISI
ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) imefafanua kuhusu mshahara wa Rais
John Magufuli ikisema kuwa mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa
umma hupangwa katika bajeti, hivyo mshahara wa Rais ni ule
ulioidhinishwa katika Bajeti ya mwaka 2015/16.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dk
Laurian Ndumbaro, bajeti ya mishahara yote ya watumishi wa umma na
viongozi wa umma hupangwa kila wakati pale bajeti inapoandaliwa na
kuidhinishwa na kwamba Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya.
“Wizara
yetu ndiyo yenye dhamana ya mishahara ya watumishi wa umma na viongozi
wa umma, na hii huandaliwa kila mwanzo wa mwaka kabla ya kuanza kwa
mwaka mpya wa fedha. Kwa hiyo mwaka 2015/16 fedha zake ziliidhinishwa
Juni mwaka jana na kuanza kutumika Julai,” alisema Dk Ndumbaro.
“Kwa
hiyo, bajeti hiyo iliidhinishwa kwa viongozi wote, Rais, Makamu wa
Rais, wabunge na watumishi wote wa umma. Hivyo, mshahara wa Rais, kwa
mantiki hiyo, Rais Kikwete (Jakaya) ndio huo ambao unatumiwa na Rais
John Magufuli. Kama mshahara, hakuna tofauti, hakuna mabadiliko, kiwango
ni kile kile. Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya,” alifafanua Katibu Mkuu huyo wa Utumishi na Utawala Bora.
Kumekuwapo
na taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari kuhusu mshahara wa Rais
na hivi karibuni, baadhi ya vyombo hivyo vilidai kuwa Rais mstaafu
Kikwete alikuwa analipwa Sh milioni 34.
HII NDO MISHAHARA YA RAIS MAGUFULI NA KIKWETE..YAWEKWA WAZI RASMI
Reviewed by The Choice
on
8:39:00 AM
Rating:
No comments: