Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimesema hakimtambui Dkt
Mohamed Ali Shein aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio
uliofanyika mwezi uliopita.
Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakizungumza kwa mara ya kwanza
tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ambao chama hicho kilisusia, wamesema
hawamtambui Dkt Shein kama rais wa visiwa hivyo.
“Tangu mapema, tangu Jecha (Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
Jecha Salim Jecha) alipofuta uchaguzi, tulisema waziwazi kwamba haikuwa
halalali. Walipoitisha uchaguzi wa marudio, tulisema waziwazi uchaguzi
huo sisi hatuutambui na tukawataka wananchi wasipige kura,” amesema
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Bw Hamad alikuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi
uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na ambao matokeo yake yalifutwa
na tume.
“Kama Rais ametokana na mchakato ambao hamkuutambua nyinyi tangu mwanzo,
sasa leo kuja kusema hatumtambui kwa nini iwe ni haramu? Hatumtambui.”
Chama hicho kimesema kitatumia njia za kidemkrasia kulalamika dhidi ya
Dkt Shein na serikali yake.
Aidha, kimeiomba jamii ya kimataifa kuwawekea vikwazo watu binafsi
waliofanikisha uchaguzi huo wa marudio ambao chama hicho kimesema
ulikuwa “uongozi haramu”.
Wiki iliyopita, Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC)
lilisitisha ufadhili wa $472milioni kwa Tanzania likilalamikia uchaguzi
visiwani Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao. Pesa
hizo zilikuwa za kutumiwa katika miradi ya kusambaza umeme
No comments: