Nay wa Mitego ajitangaza kuwa atakuwa tajiri mkubwa kuliko wote nchini Tanzania

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego baada ya kudai kuwa utajiri wake kwa sasa ni zaidi ya bilioni 1, amedai baada ya mwaka mmoja atakuwa tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote Tanzania. Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chart cha Clouds TV hivi karibuni, Nay amesema kwa sasa tayari ameshaingia kwa miguu miwili katika biashara ya kilimo.

Mimi ni mtu ambaye naishi maisha ya ukweli na sijawai kufake, kuanzia mwezi wa sita nimeshaanza kuwekeza, nafikiri hii inaweza ikawa surprise kwa mashabiki wangu. Nimeshaanza kuwekeza katika kilimo, mimi nimeshaanza kununua eka kadhaa pengine panapo majaliwa ikifika mwakani kuna uwezokano wa kuwa tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote,” alisema Nay.

Nay alidai kwa sasa nje ya muziki anaingiza pesa kupitia biashara ya daladala
Nay wa Mitego ajitangaza kuwa atakuwa tajiri mkubwa kuliko wote nchini Tanzania Nay wa Mitego ajitangaza kuwa atakuwa tajiri mkubwa kuliko wote nchini Tanzania Reviewed by The Choice on 8:11:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.