BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KISINI AREJESHWA NCHINI
Balozi Radhia Msuya
Rais
Dk. John Magufuli, amemrudisha nyumbani aliyekuwa Balozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, pamoja na watumishi wengine watano,
baada ya muda wao kumalizika.
Hii
ni mara ya pili kwa Rais Dk. Magufuli kuwarejesha nyumbani Mabalozi wa
Tanzania walioko nchi za nje baada ya muda wao wa mkataba kumalizika.
Ikumbukwe
kuwa Januari 25, mwaka huu, Rais Magufuli alimrejesha nyumbani Balozi
wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe, kuja kufanya kazi
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela
na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk. Batilda Buriani,
baada ya mikataba yao kumalizika.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dk. Augustine Mahiga, amesema kurudhishwa nyumbani kwa Balozi Msuya, ni
jambo la kawaida kwa sababu bado kazi ya kuwarudisha nyumbani Mabalozi
waliomaliza mikataba yao linaendelea.
Alisema
kwa sasa serikali inachofanya ni kuwarudisha nyumbani Mabalozi ambao
mikataba yao imemalizika na kuwapeleka watumishi wengine wakapate uzoefu
nje ya nchi.
Alisema
kuna makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni watumishi wa idara ambao
muda wao wa miaka mitano umemalizika ambao wanarudishwa nyumbani ama
kuhamishiwa kituo kingine cha kazi.
Alisema
kundi la pili ni la Mabalozi ambao siyo watumishi wa wizara, lakini
waliteuliwa na Rais kwa mkataba, hivyo mikataba yao ikimalizika Rais
mwenyewe ndiye anayeamua kama ni kuwaongezea au kusitisha na kurudi
nyumbani.
Dk.
Mahiga alitaja kundi la tatu kuwa ni Mabalozi ambao muda wao wa kukaa
nje umemalizika au umri wao wa kustaafu umefika, lakini mikataba yao
bado haijamalizika, hivyo Rais anaamua kuwarudisha nchini ili wapumzike
na wengine wakashike nafasi zao.
Alisema
kuna Mabalozi ambao mikataba yao ya kufanya kazi nje ya nchi ni miaka
mitano, lakini wamekaa zaidi ya miaka 10, hivyo serikali iko katika
mchakato wa kuwarudisha nyumbani.
BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KISINI AREJESHWA NCHINI
Reviewed by The Choice
on
8:13:00 PM
Rating:
No comments: