MSANI MASANJAASEMA ANAJIPANGA TENA KUJA KUGOMBEA UBUNGE LUDEWA
Mchekeshaji
Masanja Mkandamizaji amesema akukurupuka kuwania ubunge wa jimbo la
Ludewa, mkoani Njombe kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada
ya aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo Deogratius Filikunjombe kufariki kwa
ajali.
Akizungumza
katika kipindi cha Uhondo cha EFM Alhamisi hii, Masanja alizungumzia
kitu ambacho kilimkwamisha kupata didhaa ya kugombea ubunge kupitia
chama hicho.
“Yaani maana ya kukurupuka ni kujituka upo sehemu ambayo haukupanga kuwepo, ila mimi ile yote ni mipango,” alisema Masanja.
“Kwa
hiyo mimi niliamua kugombea lakini maandalizi yalikuwa madogo, kwa
sababu kile kifo kilitokea kwa ghafla wakati huo nipo kwenye kampeni za
mweshimiwa. Kwa hiyo baada ya kutokea tatizo hilo mimi nitarudi jimboni
na kuchukua form lakini pia watu ambao walipiga kura ni wenyeviti wa
kata, kwa sababu ulikuwa uchaguzi mdogo, sasa ile ngoma ingepigwa na
raia sasa hivi ningekuwa bungeni. Lakini bado umri wangu unaruhusu miaka
mitano ijayo nitagombea tena,” aliongeza Masanja.
Bongo5
MSANI MASANJAASEMA ANAJIPANGA TENA KUJA KUGOMBEA UBUNGE LUDEWA
Reviewed by The Choice
on
9:33:00 AM
Rating:
No comments: