MENGINE KUTOKA KWA "KIM JONG-UN" RAIS WA KOREA KASKAZINI YAKO HAPA
Kiongozi wa Korea Kaskazini
Kim Jong-un amevitaka vikosi vya taifa hilo vijiandae kutumia silaha za
nyuklia “wakati wowote”, vyombo vya habari vya serikali nchini humo
vimesema.
Ameambia viongozi wa
kijeshi kwamba North Korea itabadilisha hali yake ya kijeshi na kuwa
tayari hata kutekeleza mashambulio ya kuzuia hatari, shirika la habari
la KCNA limesema.
Lakini licha ya madai hayo, bado haijabainika taifa hilo limepiga hatua gani katika kuandaa silaha zake za nyuklia.
Umoja wa Mataifa umewekea
taifa hilo vikwazo vikali zaidi baada ya Prongyang kufanya majaribio ya
nyuklia na makombora ya masafa marefu.
Baada ya kuwekewa vikwazo, Korea Kaskazini ilijibu kwa kufyatua makombora sita ya masafa mafupi baharini.
KCNA imesema Kim alikuwa
akizungumza wakati wa zoezi la kijeshi Alhamisi. Inaaminika huo ulikuwa
wakati ambao makombora hayo yafyatuliwa.
Alisema Korea Kaskazini
“lazima iwe tayari kufaytua silaha za nyuklia wakati wowote” kwa sababu
maadui wanaitishia Korea Kaskazini.
MENGINE KUTOKA KWA "KIM JONG-UN" RAIS WA KOREA KASKAZINI YAKO HAPA
Reviewed by The Choice
on
8:19:00 PM
Rating:
No comments: