LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH

jaydee
Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Lady Jaydee amefunguka kuhusiana na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gadner G Habash.

Aliulizwa swali hilo na mtangazaji Sam Misago katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.
“Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama mimi kama Jaydee na si vinginevyo,”alisema Jaydee.
Msanii huyo ameibuka tena na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndindindi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.

CHANZO na Bongo5.

LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH Reviewed by The Choice on 8:42:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.