Ic’u Ibrah amtaka Wema Sepetu kwa gharama yoyote ile, Ni baada ya kumalizana na Shamsa Ford
Nyota wa filamu Nchini Burundi na Rwanda Ibrahim Ismael ‘Ic’u Ibrah’ amefunguka kwa kusema kuwa moja kati ya ndoto zake ni kuigiza filamu moja kubwa na Madame Wema Sepetu kwani ni msanii anayeamini kuwa ni mwigizaji mzuri na anaweza kuigiza.
“Nashukru kwa mara ya kwanza kuigiza na actress kutoka Tanzania Shamsa
Ford, lakini nitafurahi sana nitakapofanikiwa kuigiza na Wema Sepetu kwa
gharama yoyote, anajua sana mimi ni kama Kanumba vile,”anasema Ibrah.
Msanii huyo nyota raia wa Burundi amedai kuwa anazikubali sana kazi za
marehemu Steven Kanumba huku akiamini kuwa msanii huyo alikuwa bora kwa
Tanzania anatamani awe kama Kanumba katika uigizaji na hilo anaamini
kuwa atalifanya.
Ibrah ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Burundi na tayari
amefanikiwa kutayarishaji na kuigiza filamu kali na za kusisimua kama
vile Wife of my Life, Fake deal, Seconde na Questions House ambazo
zimeteka soko la filamu Burundi, Rwanda, Congo DRC na sehemu nyingine.
Ic’u Ibrah amtaka Wema Sepetu kwa gharama yoyote ile, Ni baada ya kumalizana na Shamsa Ford
Reviewed by The Choice
on
10:44:00 PM
Rating:
No comments: