HIVI NDIVYO RAIS MUSEVENI ALIVYO FURAHISHWA NA RAIS MAGUFULI ALIVYO KUTANA NAYE JIJINI ARUSHA
Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wakizungumza
na wanahabari baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo
ya Arusha Arusha, baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo
leo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki. (PICHA NA IKULU)
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Aidha, Rais Magufuli amesema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika mazungumzo
kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu
baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano
wa !7 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA

Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amekutana na kufanya Mazungumzo na
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoeri Kaguta Museveni, ambapo pamoja na
mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka
Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi nchini Uganda.
Rais
Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha leo jioni mara
baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo kesho
atahudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki, utakaofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto Jijini Arusha.
Akizungumza
baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema
wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga
hadi Uganda, kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika
Mashariki.
Amesema
bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha
ajira za watu zaidi ya 15,000.
Rais
Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia
wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki,
kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji
mali.
Aidha, Rais Magufuli amesema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
HIVI NDIVYO RAIS MUSEVENI ALIVYO FURAHISHWA NA RAIS MAGUFULI ALIVYO KUTANA NAYE JIJINI ARUSHA
Reviewed by The Choice
on
9:59:00 PM
Rating:

No comments: