FELLA AFUNGUKA JUU YA GHARAMA ANAZOTUMIA KUWATUNZA VIJANA WAKE 102 WA MKUBWA NA WANAE
Meneja wa kituo cha
kusimamia wasanii ‘Mkubwa na Wanae’ Said Fella ameeleza gharama ambazo
amekuwa akitumia katika kuendesha kituo chake.
fella-1
Akizungumza na gazeti la
Mwananchi Jumatatu hii Fella anasema kwa kuwa vijana wanaoishi kituoni
hapo ni wengi, ameamua kuwa anawahudumia kwa wiki, hivyo anajua hesabu
za wiki pekee kuwamudu kwa kila mlo na matumizi yao binafsi.
“Kwa ujumla huwa nachukua chakula kwa wiki na kwa bahati nzuri wanajipikia wenyewe,” alisema Fella.
Fella anasema aliamua
kuwafunza kujitegemea hivyo akaona ni bora wajihudumie wenyewe, hesabu
zake kwa wiki ni kiasi cha Sh360,000 ambazo hutumia kwa chakula, nauli
za shule kwa wale wanaosoma na matumizi mengine pamoja na nauli kwa wale
wanaotoka nyumbani kwao.
Pia alisema kwa kuwa huwa
haingii jikoni, bado hajajua hesabu halisi, lakini jukumu la kupika hilo
analifuatilia kuhakikisha kila kijana anajifunza kujitegemea na kuwa
msaada kwa wengine
FELLA AFUNGUKA JUU YA GHARAMA ANAZOTUMIA KUWATUNZA VIJANA WAKE 102 WA MKUBWA NA WANAE
Reviewed by The Choice
on
8:08:00 PM
Rating:
No comments: