BREAKING NEWZZZ......Chad yajiondoa mashindanoni, Stars kupata hafueni
Timu ya taifa ya Chad imejiondoa kwenye mashindano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, AFCON kwa mwaka 2017 nchini Gabon.
Chad iliyokuwa imepangwa kundi G lenye timu za Tanzania, Nigeria na Misri imelazimika kujiondoa mashindanoni sababu kubwa ikiwa ni ukosefu wa fedha uliolikumba taifa hilo.
Katika barua yake iliyotumwa kwa Shirikisho la kandanda la Tanzania, Chad imeelezea ‘ukata’ unaowakabili hali iliyopelekea kushindwa kusafiri kutoka nchini kwao kufika Jijini Dar es salaam.
Kiukweli, nchi yetu inapitia kipindi kigumu cha matatizo ya uchumi na kwa upana ushiriki wetu kwenye mashindano mbalimbali umekuwa wa kuishia njiani kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Ilieleza taarifa iloyopo kwenye barua hiyo.
Timu ya taifa ya Chad ilikuwa icheze mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania siku ya Jumatatu, yaani kesho kujitoa kwao kunaufanya mchezo huo kuota mbawa huku Tanzania ikinufaika na kujitoa kwao.
Mpaka sasa, Chad inashikilia mkia kwenye kundi lao ikiwa haina alama hata moja huku Misri ikiongoza kundi hilo ikiwa na alama 7 ikifuatiwa kwa ukaribu na Nigeria yenye alama 5 na Tanzania ikiwa na alama 4.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Jijini, D,njamena nchini Chad kati ya Tanzania ulimalizika kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 huku nahodha mpya wa Tanzania, Mbwana Samatta akikiongoza vizuri kikosi chake kwa kuwa ndiye aliyefunga bao hilo pekee lililoipa ushindi Tanzania
BREAKING NEWZZZ......Chad yajiondoa mashindanoni, Stars kupata hafueni
Reviewed by The Choice
on
5:10:00 PM
Rating:
No comments: