MREMBO MALAIKA AKANA KUHONGWA GARI HILI
Diana Exavery ‘Malaika’ Na Andrew Carlos
STAA
wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza
amefungukia gari jipya la kifahari analodaiwa kumiliki aina ya Range
Rover Sport kuwa hajahongwa kama watu wasemavyo.
Akichonga
na Showbiz, Malaika aliyewahi kubamba pia na Ngoma ya Sare Sare na
Mwamtumu alisema kuwa katika picha ambayo aliachia kwenye ukurasa wake
wa Instagram hivi karibuni ni kweli gari lake na kwamba hajahongwa na
mtu.
Range Rover Sport
“Ni
kweli lile gari ni la kwangu na nipo katika utaratibu wa
kulishughulikia litoke bandarini, sijahongwa na mtu jamani hao wanasema
tu ila mimi nimesema nilichosema inatosha,” alisema Malaika.
MREMBO MALAIKA AKANA KUHONGWA GARI HILI
Reviewed by The Choice
on
5:03:00 PM
Rating:

No comments: