Vurugu kubwa imezuka kati ya wananzengo na familia kugombea maiti Shinyanga.


 Diwani wa kata ya Kambarage iliyoko mjini Shinyanga Mh.Ramadhani Mwendapole amelazimika kuingilia kati na kuzuia vurugu kati ya wananzengo na familia ya Bw.Kalistus Shirima kugombea mwili wa marehemu Emiliani Peter Kulwa miaka 26 aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha ambapo familia hiyo ilizuia mwili wa marehemu usiagwe kwa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao moshi Kilimanjaro.
Wakizungumza kwa masikitiko wanaumoja wa kusaidiana katika shida na raha maarufu kama wananzengo wamedai kuwa wakati marehemu akiwa mgonjwa ndugu zake walikuwa wakiwazuia watu wasimujulie hali mgonjwa huku wakidai kuwa kifo cha Emiliani Kulwa kimesababishwa na uzembe wa ndugu zake kwakuwa hata alipofariki hakuna mtu yeyote aliyekuwa karibu naye na ndugu hao walikuwa katika biashara zao hadi alipotokea msamaria mwema ndipo akagundua kuwa mgonjwa ameshapoteza maisha.
 
Aidha wakati diwani wa kata ya kambarage Mh.Ramadhani Mwendapole alipoingilia kati na kutuliza ghasia hizo ndipo wanafamilia wakaamua mwili wa marehemu Emiliani Peter Kulwa uletwe mahali hapo ili uagwe kwa heshima za mwisho tayari kwa kusafirishwa kuelekea moshi kwa mazishi huku mwenyekiti wa mtaa wa Kambarage Bi.Fatuma Juma akitangaza faini ya shilingi laki tano kwa familia ya marehemu kwa kosa la kuzuia marafiki na wanazengo kumhudumia mgonjwa na kufanya uzembe unaodhaniwa kusababisha kifo cha marehemu emiliani kulwa
Vurugu kubwa imezuka kati ya wananzengo na familia kugombea maiti Shinyanga. Vurugu kubwa imezuka kati ya wananzengo na familia kugombea maiti Shinyanga. Reviewed by The Choice on 9:40:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.