STAA LADY JAY DEE AAMUA KUVUNJA UKIMYA ASEMA HAYA
Mkongwe
wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena
kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki. Lady Jaydee
ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki baada ya siku 30 kuanzia leo.
Wiki
kadhaa zilizopita Lady Jaydee aliwahi kuwaomba wapenzi wa muziki wake
kuwa wavumilivu na kuwataka wasubiri kwani kwa kipindi hicho alikiri
wazi kuwa hana kitu cha kuimba wala hakuwa na mizuka ya kuimba, kutokana
na mambo yake ya hapa na pale na kuwataka wapenzi wake kwenye muziki
kudumisha amani.
“Karibu
tu lakini sina lolote kwa sasa, sina kabisa na sitakuwa nalo kwa
kipindi kirefu sana, yaani sina, sina, sina. wapenzi huvuta subira
mashabiki huhama hama. Wapenzi vuteni subira na dumisheni amani”
Aliandika Lady Jaydee
Baada
ya ukimya na mashabiki kuanza kuhoji juu ya ukimya wake kwenye muziki,
mwanadada Lady Jaydee alikuja na kuweka wazi kuwa amekuwa kimya lakini
hawezi kufanya lolote sababu hakuwa na jambo la kusema au kuimba kwa
wakati huo na kuwataka tena mashabiki na wapenzi wa muziki wake kuwa
wavumilivu.
“Ni
kweli sijasema ,ni kweli nimekaa kimya lakini siwezi sema tu endapo
sina cha kusema mnaweza kuvumilia? Kama ninavyo vumilia? Napumzika tu
sina cha kufanya mvumilie nitarudi sema sina cha kusema na siko tayari
kusema, nitasema nikiwa tayari kusema” Alimaliza Lady Jaydee
Lady
Jaydee sasa amepata cha kusema na amepata ya kuzungumza na ndio maana
ametangaza rasmi ujio wake mpya kwenye muziki wa bongo fleva, Jide
amesema kuwa baada ya siku 30 kuanzia leo atasimama tena.
Eatv.tv
STAA LADY JAY DEE AAMUA KUVUNJA UKIMYA ASEMA HAYA
Reviewed by The Choice
on
11:38:00 PM
Rating:
No comments: