Ray kusaka ubalozi kwenye makampuni ya maji,ni baada ya ishu yake ya kunywa maji ku kiki
Baada ya kauli ya msanii wa bongo muvi Ray kigosi kuwa gumzo kila kona msanii huyo amesema amepata wazo la kufanya biasahra kupitia kiki hiyo.
Ray amesema amepata mawazo kutoka kwa watu wengi na yeye yuko kwenye mpango wa kuzungumza na makampuni yanayouza maji ili aweze kuyatangaza au anaweza kutengeneza documentary inayoelezea umuhimu wa kunywa maji na kuomba air time kwenye vituo vya televisheni
“Nimepata mawazo kutoka kwa watu wengi,ulaya ingekuwa ni kitu kikubwa lazima makampuni yangenifuata niwafanyie matangazo lakini kwetu Afrika bado..naweza kwenda kampuni yoyote kuomba sponsorship nikapata au kutengeneza documentary ya umuhimu wa maji nikapeleka kwenye TV nikapata pesa” alifunguka Ray ambapo wiki iliyopita alisema anakunywa sana maji ndio mana anakuwa mweupe kufanya kauli hiyo kuwa gumzo kwenye mitandao.
Source: Clouds
Ray kusaka ubalozi kwenye makampuni ya maji,ni baada ya ishu yake ya kunywa maji ku kiki
Reviewed by The Choice
on
4:12:00 PM
Rating:
No comments: