NUH MZIWANDA NA SHILOLE WAENDELEA KUPIGANA VIJEMBE MTANDAONI
Shilole na Nuh Mziwanda enzi wakiwa wapenzi.
Baada
ya hivi karibuni Shilole na Nuh Mziwanda kumwagana kisha kila mmoja
kumwanika mpenzi wake mpya, sasa wasanii hao imekuwa ni full
kuringishiana huku kila mmoja akidai amepata mtu sahihi
Shilole akiwa na mpenzi wake mpya.
Nuh
juzikati alisema kuwa, kwa Shilole alikuwa kapotea njia na sasa
amempata mwenza sahihi aitwaye Erah Erah huku Shilole naye akitamba
kuwa, mwanaume aliyempata ambaye anafahamika kwa jina la Medy Music ana
kila sifa ya kuwa mume tofauti na Nuh.
“Hapa nimefika, huyu sasa ndiye mume wangu,” alisema Shilole kwa kifupi.
Hata
hivyo, rafiki wa karibu wa Nuh aliitonya safu hii kuwa, kila
wanapokutana wasanii hao wakiwa na wapenzi wao inakuwa ni mwendo wa
kurushana roho tu.
NUH MZIWANDA NA SHILOLE WAENDELEA KUPIGANA VIJEMBE MTANDAONI
Reviewed by The Choice
on
12:54:00 PM
Rating:
No comments: