Nay Wamitego adai mali anazo miliki zinafikia thamani ya bilioni moja

Staa wa muziki Nay wa Mitego amedai kuwa hela anazomiliki benki pamoja na mali anazomiliki zina thamani ya bilioni 1. Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chat Show cha Clouds TV Ijumaa hii, Nay alisema biashara pamoja na muziki wake ni vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.

“Mimi mali zangu na kila kitu zinafika kwenye bilioni hivi, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara ninazofanya thamani yake zinafikia bilioni moja na kitu. Sitaki kudanganya watu sijui kwenye bilioni 2 huko,” alisema Nay.

Nay alisema hela hizo amezipata kupitia biashara ya daladala pamoja na muziki wake.

Rapa huyo mwaka 2014 alihamia kwenye nyumba yake iliyopo Mbezi jijini Dar na kudai nyumba hiyo ina thamani ya milioni 200
Nay Wamitego adai mali anazo miliki zinafikia thamani ya bilioni moja Nay Wamitego adai mali anazo miliki zinafikia thamani ya bilioni moja Reviewed by The Choice on 8:53:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.