HATIMAYE RAYUU AOLEWA PICHA ZIKO HAPA
Alice Bagenzi ‘Rayuu’ na mumewe Ahmedi Said.
Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda
Dar
es Salaam: Cherekochereko! Habari ikufikie kuwa mwigizaji wa sinema za
Kibongo aliyejipatia umaarufu baada ya picha zake za utupu kuzagaa
mitandaoni, Alice Bagenzi ‘Rayuu’, hatimaye ameolewa na mfanyabishara
mwenye asili ya Kiarabu aitwaye Ahmedi Said.
Kwa
mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Rayuu, ndoa hiyo
ilitarajiwa kufungwa kwa siri Ijumaa iliyopita nyumbani kwao, Kigogo
jijini Dar bila mwaliko wa marafiki zake ili ishu isivuje.
Baada
ya kunyetishiwa ‘ubuyu huo’, mwanahabari wetu alikula mingo jirani na
nyumbani hapo hadi cherekochereko ilipoanza ndipo akatinga ndani huku
ishu hiyo ikiwa imehudhuriwa na watu wachache bila wasanii wenzake.
Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kunasa tukio hilo mwanzo hadi mwisho,
Ijumaa Wikienda lilimbana Rayuu na kumuuliza kulikoni kuolewa kimyakimya
tena bila wasanii wenzake wa Bongo Muvi ambapo alisema hakutaka
matangazo ndiyo maana akaona bora aifanye kwa siri kwani si wote
wangefurahishwa na hatua hiyo.
“Sikualika
msanii hata mmoja maana ni ndoa ya siri, nimealika ndugu wachache tu
ila nitawaalika kwenye sherehe mwishoni mwa mwezi wa tatu.
“
Najua
wengi watashangaa wakisikia nimeolewa maana watu walikuwa wakinisema
vibaya kuwa sijatulia sasa nimewathibitishia kuwa nimetulia,” alisema
Rayuu.
HATIMAYE RAYUU AOLEWA PICHA ZIKO HAPA
Reviewed by The Choice
on
9:04:00 PM
Rating:
No comments: