HUYU NDO MBUZI MWENYE VICHWA VIWILI ALIYEZALIWA NCHINI KENYA
Mbuzi mmoja katika Kijiji
cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku
akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangazawengi walioshuhudia
huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.
Kahaso Ngumbao ambaye ndio
anamfuga mbuzi huyo alitarajia mbuzi huyo angezaa mapacha kama kawaida
yake lakini imekuwa tofauti, Wanakijiji walitaka kumuua kwa madai kuwa
ni mkosi kutokana na mila za jamii hiyo.
Kwa sasa mwenye mbuzi huyo kuamua kumpeleka mbuzi wake Makao makuu ya Kilimo kwa ajili ya kumhifadhi wanakijiji wasimuue.
“Nilikuwa natafuta njia ya
kupatia msaada wa huyu mnyama maana hawezi na nikiachiwa mimi huenda
nikashindwa saa nyingine.. nikiachia watoto hawawezi kumlea vile ambavyo
labda ningekuwa mimi mwenywe” — Kahaso Ngumbao
Afisa wa Kilimo, Wanyama na Samaki aliahidi kuwa Serikali ya kaunti hiyo itatafuta mahali mbadala na kumhifadhi mbuzi huyo.
HUYU NDO MBUZI MWENYE VICHWA VIWILI ALIYEZALIWA NCHINI KENYA
Reviewed by The Choice
on
7:38:00 AM
Rating:
No comments: