HIVI NDIVYO USHUJAA WA POLISI WA DAR..WALIVYO PAMBANA NA MAJAMBAZI WALIO VAMIA BANK NA KUFANIKIWA KUWAUA
Majambazi ambao idadi
yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za kisasa jana
walivamia Benki ya Access tawi la Mbagala ambako walipora viroba
vya fedha, kuua mlinzi na baadae wanne kati yao waliuawa na
jeshi la polisi.
Watu walioshuhudia
tukio hilo walisema baada ya majambazi hao kufika katika benki
hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane mchana,yalimuua mlinzi
wa benki hiyo, kusha kubomoa kwa risasi mlango wa vioo na
kuingia ndani na kuzua taharuki kubwa
Mashuhuda hao
walisema, katika tukio hilo lililodumu kwa karibu saa moja,mmoja
wa majambazi hao aliyekuwa amevaa kininja,alikuwa barabarani
akiamuru magari kupita haraka huku akifyatua risasi hovyo.
Ilielezwa kuwa, jambazi
huyo aliyeonekana kuwa na uzoefu wa matumizi ya bunduki
alikuwa akifyatua risasi kwa kutumia mkono mmoja na ndiye
aliyewajeruhi baadhi ya wapita njia.
Hivyo,wakati uporaji
ukiendelea na jambazi huyo akiimarisha ulinzi barabarani baadae
hakukuwa na magari wala pikipiki zilizokuwa zikipita.
Mfanyabiashara wa duka
la vifaa vya ujenzi jirani na benki hiyo,Ramadhani Tairo
alisema baada ya jambazi huyo kuliona gari la polisi likielekea
eneo la tukio,alifyatua risasi na kulipiga kabla halijafika.Gari
hilo lilipoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni.
Tairo alisema mbali
na jambazi huyo kulipiga risasi gari la polisi pia alilirushia
bomu la mkono,lakini liliangukia barabarani bila kuripuka.Polisi
walifanikiwa kulilipua bomu hilo baadae likiwa halijasababisha
madhara kwa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo.
Mkazi mwingine wa
eneo hilo,Rebecca Maliva alisema majambazi walioingia ndani ya
benki hiyo walioneka wakitoka na viroba vitatu vya fedha ambavyo
walivipakata kwenye pikipiki na kuondoka kwa kasi kuelekea
Mkuranga kupitia barabara ya Kilwa.
Rebecca alisema polisi
zaidi walifika kwenye eneo hilo wengine wakiwa kwenye pikipiki
na kuanza kuwafukuza majambazi hao ambapo walipofika eneo la
shule ya St. Marry's,walitupa kiroba kimoja cha fedha ambacho
wananchi waliokuwa jirani waligombania na kuchukua fedha
zilizokuwemo na kisha kila mmoja kukimbia na burungutu la
noti.
Baada ya nusu saa
wakati umati ukiwa bado upo kwenye benki hiyo,magari ya polisi
yalipita katika eneo hilo yakitokea eneo la Mkuranga yakiwa
yamebeba miili ya majambazi yaliyouawa.
Magari hayo yalikuwa yakisindikizwa na vijana wa bodaboda waliokuwa wakishangilia kazi iliyofanywa na polisi.
Kamanda wa p[olisi
kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alizungumzia kwa ufupi
tukio hilo n kwamba majambazi manne yaliuawa na kukamata silaha
tatu,lakini hakutaka kuingia kwa ndani akisema atatoa taarifa
zaidi leo
HIVI NDIVYO USHUJAA WA POLISI WA DAR..WALIVYO PAMBANA NA MAJAMBAZI WALIO VAMIA BANK NA KUFANIKIWA KUWAUA
Reviewed by The Choice
on
2:05:00 PM
Rating:
No comments: