HATIMAYE DINNA MARIOS AELEZEA JINSI ALIVYO POTEZA KIPINDI CHAKE CHA LEO TENA CLOUDS FM..NA KUKUTA ASHAWEKWA MTU MWINGINE
Nilipompata Zion kama mzazi yoyote ilikuwa ni furaha sanaa alileta furaha maishani mwangu na mwanzo mpya katika maisha yangu.
Katikati maisha yangu yoote nilikuwa
muoga sanaa kupata mtoto sikuwa najua nitaanzia wapi kumlea.Zile story
za wakinamama waliotangulia kuwa kuzaa kunauma zilikuwa zinanipa stress
saana.
Lakini Nilimuomba Mungu nikifikisha
miaka 30 Mungu anijaalie mtoto katika mahusiano yanayoeleweka.Zion
hakuwa bahati mbaya siku ambayo baba yake alisema anatamani tupate mtoto
Mungu aliweka tiki matamanio hayo wiki iliyofuata nilishika ujauzito.
Nikiwa natimiza miaka 30 nilikuwa na mimba kubwa ya Zion na nikamzaa nikiwa na miaka 30 nikaamini ni mpango wa Mungu.
Nilipopoteza leo tena nilihuzunika
sana nikaanza kukufuru Mungu.Kwamba kwa miaka 8 mfululizo nimekilea
kipindi leo nimeenda kujifungua narudi nakuta nafasi hiyo haipo kwa
nini?kwa nini kuzaa kubadilishe tena ghafla?nakumbuka siku hiyo hata
kunyonyesha sikuweza kabisa kabisa
Lakini nikamuomba Mungu anipe
muongozo anataka kunipeleka wapi?Kwa sababu ya Zion niliweza kuja na
product ya mafuta ya nazi dina marios coconut baby oil.
Alipotimiza mwaka mmoja picha za
birthday yake ndio zilileta wazo la kuanzisha magazine ya
parenting/malezi .Later nikajoin @efm_93.7 radio nakuanza kipindi kipya
cha UHONDO.
Nilianza upya na MTOTO wangu Zion
ndio inspiration ya mwanzo wangu mpya.Baada ya mwaka mmoja kupita wa
kulipika wazo jana nikafanikiwa kutambulisha magazine ya MTOTO kwa
ndugu,jamaa na marafiki waliokuja katika birthday party ya Zion.
Na magazine cover story toleo la
kwanza yupo Zion na mimi mama yake kukusimulia mengi maana yeye ndio
inspiration ya hiyo magazine.
Lolote tunalomuomba Mungu atatupa lakini sio kwa picha ile tunayoitaka ni kwa namna apendavyo yeye na anavyoona inakufaaa.
Usikose nakala ya MTOTO magazine kuanzia wiki ijayo kusoma mengi yahusuyo malezi ya watoto wetu . Litauzwa Tsh 5,000 tu!
HATIMAYE DINNA MARIOS AELEZEA JINSI ALIVYO POTEZA KIPINDI CHAKE CHA LEO TENA CLOUDS FM..NA KUKUTA ASHAWEKWA MTU MWINGINE
Reviewed by The Choice
on
9:52:00 PM
Rating:
Hiyo ndio maana Halisi ya Maisha
ReplyDelete