DIRECTOR HANSCANA AZIDI KUMTUPIA VIJEMBE MSANII Q CHILLA
Muongozaji
wa video nchini Hanscana, amemjibu Q Chief kuhusu tuhuma alizowarushia
directors wa video wa bongo kwamba hawana lolote na hawezi fanya nao
kazi tena.
Akizungumza katika kipindi cha Planet
Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Hanscana amesema Q Chief ana
stress za maisha ndio maana amekuwa akiongea ovyo.
“Ye ana stress za maisha, haiwezekani
ukafanya muziki zaidi ya miaka 17 halafu huna hata pikipiki wakati kuna
watoto wamekuja tu juzi kirahisi rahisi alafu wana kila kitu,” alisema
Hanscana.“Kwa hiyo lazima upate
mastress uanze kutapatapa, si unajua mfa maji, u can see ur self jamaa
ana more than 17 yrs in the game alafu he got nothing, halafu kuna
watoto tu wadogo wanafanya kitu, kwa hiyo unaweza ukafikiria, suala dogo
kama hilo kitaalamu hizo ni stress za maisha,” aliongeza Hanscana.
Pia Hanscana amemtaka Q Chief akae pembeni na kuwaachia wasanii wachanga wafanye kazi kwa sasa, na yeye abaki kuwa mtazamaji.
“Ninachomshauri atuachie tu new
generation tufanye vitu vyetu , tuna mwaka mmoja ndani ya game tuna
drive, tunaishi vizuri, atuache tu vijana aangalie tu game awe
anatuangalia Youtube,” alisema Hanscana.
DIRECTOR HANSCANA AZIDI KUMTUPIA VIJEMBE MSANII Q CHILLA
Reviewed by The Choice
on
8:25:00 AM
Rating:
No comments: