BREAKING NEWS : AJALI MBAYA YA BASI LA MASHIMBA LAGONGANA NA GARI DOGO
Watu
wanne wamefariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express
lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na
gari dogo katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu Mkoani
Shinyanga
Ajali
hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa
ilisababishwa na gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo
ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu wawili waliokuwa
katika gari hilo akiwemo dereva walifariki dunia papo hapo
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George
Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo
walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni
wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.
Hata
hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka
kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi
walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.
Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi
BREAKING NEWS : AJALI MBAYA YA BASI LA MASHIMBA LAGONGANA NA GARI DOGO
Reviewed by The Choice
on
10:44:00 AM
Rating:
No comments: