WAZIRI NAPE AFUNGIA KIWANDA BUBU UWANJA WA TAIFA

download (1)
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amekifunga mara moja kiwanda kilicho kuwa kikiendeshwa kwa njia zisizo halali na  Wakandarasi wa  Uwanja wa Taifa,  Kampuni ya BFG kutoka nchini China.

Mhe. Nape amefanya zoezi hilo leo  baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya Uwanja wa Uhuru na kubaini kuwepo kwa kiwanda hicho ambacho ni kinyume na taratibu na mkataba wa kisheria walio ingia baina ya Serikali na Kampuni yao ambao unahusu ujenzi wa miudombinu ya michezo pekee ikiwemo  Uwanja wa Taifa na Uhuru.
Kabla ya kukifungia kiwanda hicho Waziri Nape aliomba maelezo ya kina juu ya uhalali wa uwepo wake na namna uendeshwaji wake unavyofanyika ili kujiridhisha ndipo alipofikia uamuzi huo wa kukifungia baada ya kujiridhisha kuwa kinaendeshwa kinyume na utaratibu.
“Ninataka kujua kwa undani zaidi uhalali wa kiwanda hiki cha useremala kama kipo ndani ya mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na eneo changamani la michezo”. Alisisitiza Nnauye
Uwepo wa kiwanja hicho kunapelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa maboresho na ujenzi wa Uwanja wa Uhuru.
Aidha Waziri Nape amemuagiza Meneja wa Uwanja wa Taifa Rishe Urio kutoa maelezo ya kina juu ya uwepo wa Kiwanda hicho katika eneo la ndani ya masaa 24 ni kwanini akutoa taarifa juu ya uwepo wa shughuli za Kiwanda hicho katika eneo hilo ila hali yeye ndiye msimamizi mkuu wa Uwanja huo.
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya BFG Cheng Longhai amekiri kuwa Kiwand hicho kinaendeshwa kinyemela kwakuwa hakihusiani na mkataba wa kampuni hiyo.
Wakatihuohuo Nape ameuagiza uongozi wa Selcom Tz kuhakikisha inakimilisha mfumo wa Tiketi za Kielekroniki na kukabidhi kwa Serikali ndani ya siku 30 kuanzia sasa.
Agizo hilo ni muendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim wakati akiongea na wadau wa sekta ya michezo kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu.
WAZIRI NAPE AFUNGIA KIWANDA BUBU UWANJA WA TAIFA WAZIRI NAPE AFUNGIA KIWANDA BUBU UWANJA WA TAIFA Reviewed by The Choice on 6:51:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.