Mshiriki wa Big Brother Africa, Feza Kessy amejiunga na kituo cha redio, Choice FM cha Dar es Salaam. Feza atakuwa akitangaza kipindi cha Hard Drive kinachoanza saa 12 asubuhi hadi saa 3 akiwa na Sebastian Mwaikambo. Hivi karibuni Feza aliachia video ya wimbo wake, Sanuka aliomshirikisha Chege.
No comments: