MAJAMBAZI WATATU WAUAWA NA JESHI LA POLISI HUKO KAHAMA
Jeshi la Polisi
wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi watatu
yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel
Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza kujibizana
risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na kufika katika
eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita Kawawa, amesema katika tukio hilo raia
mwingine mmoja alipigwa risasi na majambazi hao na kupoteza maisha
wakati akipelekwa hospitali huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi
nzuri waliyoifanya.
Akizungumza kwa njia ya simu kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde wanapoona dalili zozote
za kiuhalifu zinafanyika.
Katika tukio hilo jeshi polisi
limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja aina ya Short Gun na moja ya
kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi
sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili za bunduki.
MAJAMBAZI WATATU WAUAWA NA JESHI LA POLISI HUKO KAHAMA
Reviewed by The Choice
on
8:48:00 PM
Rating:
No comments: